Na Hokelai Aterio Shemtoi Mganga
Ni mwaka kupanga Tanzania ya baadae
iweje. Ni mwaka wa kupanda mbegu bora, mwaka ambao tukizubaa, tukilala
tu lazima tutavuna mabua. Haswa ukizingatia nchi yetu inapita kwenye
kipindi kigumu cha historia kutengeneza KATIBA mpya na pia tathimini
pana juu ya wagombea URAISI wa mwaka 2015. kaka Maggid Mjengwa aliita
nchi ya Wasadikika, hawana mpango wa kuwaza kuhusu katiba iliyopo, mpaka
sasa kuna baadhi ya watu hawajui chochote kuhusu katiba zaidi kelele za
"serikali tatu tu"Asilimia kubwa ya Watanzania ni vijana na watoto,
ambao Vijana hao kazi yao kubwa ni kubishana kwenye facebook na twitter
na kushabikia nguo za vyama, mara gwanda huyu kijani mara yule vidole
viwili. Sasa ikifika kipindi cha kuvuna tutakapovuna mabuha tusije
kujilaumu. Mungu azidi kuibariki Tanzania na Mungu azidi kuwabariki watu
wa Tanzania. Nawatakia kheri ya Mwaka Mpya wa 2014. Saturday, 4 January 2014
HOME »
» MWAKA 2014 NI KUIJENGA TANZANIA YETU KWA MAENDELEO YETU
0 comments:
Post a Comment