Aida Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha
Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua
watoto wanne mapacha kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia
Mwaka mpya anaendelea vizuri.
Mwanamke
huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya
Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua majira ya saa
10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya
Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito wa kawaida tofauti na
matarajio ya Wengi. Muuguzi
na msimamizi wa Watoto katika chumba cha Joto Sista Frolence Maisa
amesema hali za watoto ni nzuri ambapo mama mzazi anahitaji kupatiwa
vyakula vinavyoweza kumuongezea maziwa mengi kutokana na idadi ya watoto
aliyonayo kikosi cha blog ya Mbeya yetu Kikiongozwa na Joseph Mwaisango ambacho kilifika kumjulia hali kiliguswa na hali hiyo na kujitolea kamsaada kidogo wa nguo za watoto sabuni chupa na dishi hivyo kuwaomba wadau wengine kumsaidia mama huyo ili aweze kuwalea vizuri watoto wake. Katibu msaidizi wa hospitali ya Rufaa Mbeya Mwansasu akipokea msaada huo kwa niaba ya mzazi
KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida
Mwanamke mmoja, Aida Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya
Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua watoto wanne mapacha kwa
mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya anaendelea
vizuri.
Mwanamke
huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya
Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua majira ya saa
10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya
Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito wa kawaida tofauti na
matarajio ya Wengi.
Kwa
mujibu wa Muguuzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mbozi aliyemfanyia huduma
mwanamke huyo, Grace Konga alisema mzazi huyo ni miongoni mwa wazazi 9
waliojifungua katika Mkesha wa Mwaka mpya huku yeye akivunja rekodi kwa
kujifungua watoto wanne kwa njia ya kawaida.
Muuguzi
huyo alisema watoto hao walizaliwa wakiwa na uzito uliotofautiana kwa
mtoto wa kwanza hadi wa mwisho kuanzia kilogramu 1.6,1.5,1.5 na 2.0
ambapo baada ya kuona hali hiyo ilibidi kumpa rufaa kwa ajili ya msaada
zaidi katika Hospitali ya wazazi ya Meta ambapo wapo katika Chumba cha
Joto hadi sasa.
Aidha
kwa mujibu wa Muuguzi na msimamizi wa Watoto katika chumba cha Joto
Sista Frolence Maisa amesema hali za watoto ni nzuri ambapo mama mzazi
anahitaji kupatiwa vyakula vinavyoweza kumuongezea maziwa mengi kutokana
na idadi ya watoto aliyonayo.
Alisema
kwa hivi sasa watoto wananyonya vizuri amb po maziwa yakipungua kwa
mama itahitajika msaada wa maziwa ya Kopo aina ya Laktojeni ili watoto
waendelee kupatiwa maziwa kama kawaida na afya zao kuimarika.
Kwa
upande wake Mzazi wa watoto hao Aida Nakawala alisema hali yake kiuchumi
siyo nzuri kuweza kumudu kuwalea watoto hao na kuongeza kuwa mume wake
ni mkulima aliyemtaja kwa jina la Web Simkanda hivyo anaomba msaada wa
hali na mali kutoka kwa wasamaria wema.
Alisema
huo ni uzao wake wanne ambapo mtoto wake wa kwanza anaumri wa miaka
saba, anayefuata ana miaka miwili na miezi tisa huku mwingine akiwa
amefariki dunia mara baada ya kujifungua kabla ya uzao huu unaofanya
kuwa na watoto Sita.
Alipoulizwa
kuhusu kuwepo kwa hali kama hiyo ya kujifungua watoto zaidi ya mmoja
katika familia yao alisema Mama yake mzazi amewahi kujifungua mapacha
wawili tu na hakuna mtu mwingine aliyewahi kuzidisha idadi hiyo ya
watoto kama yeye.
Hata hivyo kutokana na kuguswa kwa
mahitaji ya binti huyo na wanawe kikosi cha blog ya Mbeya yetu ambacho
kilifika kumju ulia hali kiliguswa na hali hiyo na kujitolea kamsaada
kadogo hivyo kuwaomba wadau wengine kumsaidia mama huyo ili aweze
kuwalea vizuri watoto wake.
Chanzo mbeya yetu
0 comments:
Post a Comment