Rais wa Uganda, Yoweri Museveni
amekataa kuidhinisha mswada ambao ikiwa utaidhinishwa utatoa adhabu kali
kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Museveni amemuandikia spika wa bunge
barua na kumkosoa kwa hatua ya kupitisha mswada huo Disemba mwaka jana
bila ya kuwa na idadi ya kutosha ya wabunge.
Aidha Rais amesema kuwa Watu
wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja ni watu wenye akili timamu na
wanaweza kuokolewa kutokana na tabia hiyo.
Mswada huo unatoa adhabu kali kwa watu
watakaopatikana na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja ikiwemo
kufungwa jela na pia ni uhalifu kwa mtu yeyote kukosa kuripoti visa vya
mapenzi ya jinsia moja.
Mwandisi wa BBC mjini Kampala Cathrene
Byaruhanga anasema kuwa mswada huo pia unapendekeza kuadhibiwa kwa watu
wanaozungumzia maisha ya wapenzi wa jinsia moja bila ya kuwakashifu
kwani wanaweza kufungwa jela.
Kwa mujibu wa gazeti la Monitor, Rais
Museveni amesema kwamba mswada huo ulishinikizwa zaidi kupitishwa na
wabunge licha ya kuwashauri kusubiri hadi serikali itakapoutathmini.
Rais anaelewa kwamba ikiwa
atauidhinisha mswada huo na kuufanya sheria kutakua na ukosoaji mkubwa
kutoka kote hali inatakayochangia baadhi ya nchi za kigeni kusitisha
msaada kwa Uganda
0 comments:
Post a Comment