Monday, 20 January 2014

MTU MMOJA MKOANI IRINGA MATATANI KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA MIWILI

RPC -Mungi

MWANDISHI ,DIANA BISANGAO WA  IRINGA

JESHI  la polisi mkoani Iringa linamshikilia Eliabu Myogile (17) mkazi wa Gangilonga kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka miwili.
 
Akizungumza na mtandao huu    ofisini kwake leo Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea tarehe 19 januari mwaka huu.
 
Kamanda Mungi alisema mtuhumiwa huyo alimbaka mtoto wa kike jina limehifadhiwa na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri, chanzo cha tukio hilo la ubakaji ni tama ya mwili.
 
Mbali na tukio hilo la ubakaji Kamanda Mungi alisema wachumaji wa chai walioajiriwa pamoja na vibarua wa kiwanda cha chai Kilima estate kilichopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa walifanya mgomo na kuharibu mali mbalimbali za kiwanda hicho.
 
Mungi alisema chanzo cha mgomo huo ni wafanyakazi kulipwa mshahara mdogo ambao ulipelekea wafanyakazi hao kuiba mifuko ya saruji na mabati yaliyohifadhiwa stoo, katika tukio hilo hakuna binadamu yeyote aliyedhuhurika.

Watu watatu wafariki dunia katika na wengine kumi kujeruhiwa katika matukio mawili tofauti likiwemo la mtoto Yusta Mkonda (10) mkazi wa kijiji cha Migoli mkoani Iringa kutumbukia kisimani.

Akizungumza na mtandao huu  ofisini kwake leo Kamanda wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea tarehe 17 januari  majira ya saa 12 kamili jioni.
Kamanda Mungi alisema mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Mtera alitumbukia kisimani alipolkuwa akichota maji.

Wakati huohuo watu wawili wafariki dunia na wengine kumi kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wamepanda kuacha njia na kupinduka maeneo ya kijiji cha Ifwagi wilaya ya Mufindi.

Kamanda Mungi aliwataja marehemu ni Isack Ngozi (25) pamoja na Paul Mbalinga (23) ambao walikuwa wamepanda gari aina ya isuzu forward lenye namba za usajili T 478 ABX mali ya O. Mwidani lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyejulikana kwa jina moja la Nuhu.

Mungi alisema majeruhi kumi waliokuwemo katika gari hilo walilazwa katika Hospitali ya Mafinga huku dereva wa gari alikimbia mara baada ya ajali.

 

Related Posts:

0 comments: