Saturday, 18 January 2014

MTANGAZAJI WA BBC KOMLA DUMOR AMEFARIKI DUNIA GHAFLA



Komla Dumor presenting Focus on Africa 17/01/2014
Mtangazaji wa BBC  Komla Dumor amefariki dunia ghafla akiwa na umri wa miaka 41. Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi, Amin ( R.I.P Komla Dumor)

Komla na Morgan Tsvangirai katika studio za BBC London
kwa Taarifa zaidi ni kwamba 
Mwandishi  huyo wa BBC Komla Dumor amefariki ghafla nyumbani kwake kutokana na mshtuko wa moyo.
Alikuwa na miaka 41 alipopata mauti yake.Komla Dumor ameelezewa kuwa miongoni mwa waandishi shupavu barani Afrika.
Rais wa Ghana John Dramani Mahama amemtaja marehemu kama zawadi ya Ghana ulimwenguni na kuongezea kuwa Ghana imempoteza mmoja wa wajumbe wake.
Komla hivi karibuni alikuwa anaongoza kipindi cha Runinga kinachozungumzia maswala ya Afrika baada ya kufanya kazi katika radio mmoja nchini Ghana na vilevile radio ya BBC.
Muhariri wa habari za ulimwengu Andrew Whitehead amemtaja kuwa mwadishi shupavu aliyekuwa na uhusiano mzuri na wasikilizaji.
chanzo bbcswahili

Related Posts:

0 comments: