Sunday, 12 January 2014

LIGI KUU ENGLAND: ,MAN CITY YAICHAPA NEWCASTLE YAPAA KILELENI KESHO ARSENAL

 CITY YAICHAPA NEWCASTLE NA KUIPIKU CHELSEA KILELENI!!
 LIVERPOOL NAYO YAICHAPA STOKE CITY

RATIBA/MATOKEO:
[Saa za Bongo]
Jumapili Januari 12
Newcastle 0 Man City 2
 Stoke 2 V Liverpool 5
Jumatatu Januari 13
2300 Aston Villa V Arsenal

BPL2013LOGOManchester City wamepanda kileleni mwa Msimamo wa Ligi Kuu England baada hii leo kuifunga Newcastle Bao 2-0 Uwanjani Saint James Park.
Edin Dzeko ndie aliewapa City Bao la kuongoza katika Dakika ya 8 na Cheick Tiote kusawazisha kwa Bao safi kwa Shuti la mbali na kukataliwa kwa utata kwa sababu Yoan Gouffran, ambae hakugusa Mpira huo, kudaiwa ni Ofsaidi na allikuwa akimziba Kipa Joe Hart.
Mara mbili Yohan Cabaye alikaribia kufunga kwa upande wa Newcastle lakini ni Alvaro Negredo ndie aliehakikisha ushindi kwa City kwa kupiga Bao la Pili katika Dakika za Nyongeza na kuing’oa Chelsea kileleni.
Jumatatu Usiku, waliokuwa Vinara kabla ya Mechi za Jana, Arsenal, wana Nafasi ya kutwaa tena uongozi ikiwa wataifunga Aston Villa huko Villa Park.
Aston Villa ndio iliyoikung’uta Arsenal Bao 3-1 huko Emirates katika Mechi ya Kwanza kabisa ya Ligi Msimu huu.
VIKOSI:
Newcastle: Krul; Santon, S.Taylor, Williamson, Yanga-Mbiwa; Anita, Tiote, Cabaye; Sissoko, Remy, Gouffran.
Akiba: Elliot, Haidara, Gosling, Marveaux, Sammy Ameobi, Ben Arfa, Cisse.
Man City: Hart, Zabaleta, Kompany, Demichelis, Kolarov; Nasri, Fernandinho, Yaya Toure, Silva; Negredo, Dzeko.
Akiba: Pantilimon, Richards, Lescott, Clichy, Garcia, Milner, Navas.
Refa: Mick Jones
MSIMAMO:
NA TIMU P GD PTS
1 Man City 21 36 47
2 Chelsea 21 21 46
3 Arsenal 20 21 45
4 Everton 21 15 41
5 Tottenham 21 1 40
6 Liverpool 20 23 39
7 Man Utd 21 11 37
8 Newcastle 21 2 33
9 Southampton 21 4 30
10 Hull 21 -5 23
11 Aston Villa 20 -6 23
12 Stoke 20 -11 22
13 Swansea 21 -4 21
14 West Brom 21 -5 21
15 Norwich 21 -18 20
16 Fulham 21 -24 19
17 West Ham 21 -10 18
18 Cardiff 21 -18 18
19 Sunderland 21 -15 17
20 Crystal Palace 21 -18 17

Related Posts:

0 comments: