Saturday, 18 January 2014

LEO BIG MECHI STAMFORD BRIDGE: CHELSEA v MAN UNITED ANGALIA VIKOSI VITAKAVYO CHEZA LEO

>>MECHI KUANZA SAA 1 USIKU BONGO TAIMU!
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumapili Januari 19
1630 Swansea v Tottenham
1900 Chelsea v Man United
PATA DONDOO MUHIMU:
Hali za Timu:
MOYES_v_MOURINHOKiungo wa Chelsea Frank Lampard huenda akarudi baada kukosa Mechi tangu Januari Mosi akijiuguza Musuli za Mguu lakini Fulbeki wa Kulia, Branislav Ivanovic, huenda akaikosa Mechi baada kurudi Mazoezini Juzi Ijumaa baada kupona Goti lake.
Mchezaji mpya wa Chelsea, Kiungo Nemanja Matic aliesainiwa Juzi kutoka Benfica, hataanza Mechi hii kwa mujibu wa Meneja Jose Mourinho.
Nae Meneja wa Man United, David Moyes, amethibitisha kuwa Mastraika wake hatari, Wayne Rooney na Robin van Persie, hawamo kwenye Kikosi kuilichosafiri kwenda London licha ya kupona maumivu yao.
Wakati Man United wanasaka ushindi wao wa Sita katika Mechi 7 za Ligi zilizopita, Jose Mourinho na Chelsea yake inataka kudumisha Rekodi ya Meneja huyo ya kutofungwa Uwanjani Stamford Bridge kwenye Mechi ya Ligi katika himaya zake mbili Klabuni hapo kuanzia ile ya Mwaka 2004 mpaka 2007 na hii ya kuanzia Msimu huu.
Lakini Msimu uliopita, kwenye Mechi kama hii ya Ligi, Man United walimaliza ukame wa Miaka 10 kutoshinda Stamford Bridge katika Ligi Kuu baada Javier Hernandez ‘Chicharito’ kutoka Benchi na kupachika Bao la ushindi.
Mapema Mwezi Agosti, huko Old Trafford, Man United na Chelsea zilitoka Sare ya 0-0 kwenye Mechi ya Kwanza ya Ligi.
VIKOSI VINATARAJIWA:
CHELSEA (Mfumo unaweza kuwa: 4-2-3-1): Cech; Azpilicueta, Cahill, Terry, Cole; Luis, Ramiers, Willian, Oscar, Hazard; Torres.
Majeruhi: Van Ginkel (Goti).
Kupimwa kabla Mechi: Ivanovic (Goti), Lampard (Musuli za Mguu).
MAN UNITED (Mfumo unaweza kuwa: 4-2-3-1): De Gea; Rafael, Smalling, Vidic, Evra; Fletcher, Carrick; Valenica, Januzaj, Kagawa; Welbeck.
Majeruhi: Fellaini (Mkono), Ferdinand (Goti), Rooney (Nyonga), Van Persie (Paja),
Kupimwa kabla Mechi: Phil Jones (Goti), Ashley Young (Bega). 
Refa: Phil Dowd [MECHI: 15, Kadi Nyekundu: 0 Kadi za Njano:65]
TAKWIMU MUHIMU:
-Man United wameshinda Mechi 5 tu kati ya 20 za Ligi Kuu Uwanjani Stamford Bridge.
-Katika Mechi 10 zilizopita Man United wameifunga Chelsea mara 5, Sare 3 na Kufungwa 2.
MECHI 3 ZILIZOPITA ZA LIGI STAMFORD BRIDGE:
2012/13: Chelsea 2-3 Manchester United
Manchester United walimaliza ukame wa Miaka 10 kutoshinda Stamford Bridge katika Ligi Kuu baada Javier Hernandez ‘Chicharito’ kutoka Benchi na kupachika Bao la ushindi.
2011/12: Chelsea 3-3 Manchester United
Hernandez tena aliokoa Man United kwa kusawazisha Bao walipotoka nyuma kwa Bao 3-0 na kupata Sare ya 3-3.
2010/11: Chelsea 2-1 Manchester United
Penati ya Frank Lampard iliipa Chelsea Bao la kusawazisha baada Wayne Rooney  lakini David Luiz akafunga Bao lake la kwanza kwa Chelsea na kuipa ushindi. Nemanja Vidic alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu katika Dakika za Majeruhi.
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Arsenal
22
24
51
2
Man City
22
38
50
3
Chelsea
21
21
46
4
Liverpool
22
25
43
5
Everton
21
15
41
6
Tottenham
21
1
40
7
Man Utd
21
11
37
8
Newcastle
22
4
36
9
Southampton
22
4
31
10
Aston Villa
22
-7
24
11
Hull
22
-6
23
12
Norwich
22
-17
23
13
Stoke
22
-14
22
14
Swansea
21
-4
21
15
West Brom
21
-5
21
16
Crystal Palace
22
-17
20
17
Fulham
22
-26
19
18
West Ham
22
-11
18
19
Sunderland
22
-15
18
20
Cardiff
22
-21
18
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumatatu Januari 20
2300 West Brom v Everton
Jumanne Januari 28
2245 Man United v Cardiff
2245 Norwich v Newcastle
2245 Southampton v Arsenal
2245 Swansea v Fulham
2300 Crystal Palace v Hull
2300 Liverpool v Everton
Jumatano Januari 29
2245 Aston Villa v West Brom
2245 Chelsea v West Ham
2245 Sunderland v Stoke
2245 Tottenham v Man City

Related Posts:

0 comments: