Muda mchache baada ya mchezo wa jana wa ligi kuu ya England kati ya
Arsenal dhidi ya Liverpool, ambao uliisha kwa matokeo ya Liverpool
kuiadhibu Arsenal 5-1, golikipa wa klabu ya Arsenal Wojciech Szczesny
alitumia akaunti yake ya mtandao wa Twitter kuwaomba msamaha mashabiki
wa timu hiyo kwa kipigo hicho.
Aliandika: “Ilikuwa ni aibu kubwa, samahani kwa yoyote aliyekaa dakika zote kuangalia mchezo ule.”
0 comments:
Post a Comment