Saturday, 15 February 2014

FA CUP: SUNDERLAND YA KWANZA KUTINGA ROBO FAINALI!!

  >>BAADAE LEO NI CARDIFF v WIGAN, MAN CITY v CHELSEA!!


>>JUMAPILI NI ARSENAL v LIVERPOOL!!

FA CUP
Raundi ya Tano
RATIBA/MATOKEO:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Februari 15
Sunderland 1 Southampton 0
1800 Cardiff v Wigan
Sheffield Wednesday v Charlton [IMEAHIRISHWA-Uwanja umejaa Maji ya Mvua]
2015 Man City v Chelsea

SUNDERLAND 1 SOUTHAMPTON 0
FA_CUP_2013-2014Kigongo cha Mita 25 cha Craig Gardner katika Dakika ya 49 Leo huko Stadium of Light kimewapa Sunderland ushindi wa Bao 1-0 walipocheza na Southampton kwenye Mechi ya Raundi ya Tano ya FA CUP.
Ushindi huu umewaingiza Sunderland kwenye Robo Fainali na watamjua Mpinzani wao hapo kesho kwenye Droo itakayofanyika Usiku.
VIKOSI:
Sunderland: Ustari, Celustka, Dossena, O’Shea, Vergini, Cattermole, Larsson, Giaccherini, Gardner, Scocco, Borini
Akiba: Ki, Wickham, Colback, Mannone, Alonso, Roberge, Mavrias.
Southampton: K. Davis, Clyne, Yoshida, Hooiveld, Shaw, Wanyama, S. Davis, Ward-Prowse, Lallana, Guly, Lambert
Akiba: Gazzaniga, Schneiderlin, Fonte, Rodriguez, Cork, Chambers, McQueen.
Refa: Mike Dean.

FA CUP
Raundi ya Tano
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumapili Februari 16
1630 Everton v Swansea
1800 Sheffield United v Nottingham Forest
1900 Arsenal v Liverpool
Jumatatu Februari 17
2245 Brighton v Hull

THE FA CUP WITH BUDWEISER
MSIMU 2013-14
TAREHE ZA RAUNDI:
-RAUNDI YA 6: Jumamosi Machi 8
-NUSU FAINALI: Jumamosi Aprili 12 & Jumapili Aprili 13
-FAINALI: Jumamosi Mei 17

Related Posts:

0 comments: