Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Singida.
Na Nathaniel Limu, Singida
DIWANI
wa kata ya Unyambwa (CCM) Halmashauri ya Manispaa ya Singida,Shaban
Salum Satu amepandishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Singida
akituhumiwa kuwatolea lugha ya matusi maafisa wa Polisi ikiwemo kudai ni
‘mizigo’.
Diwani
huyo alifikishwa mahakamani kwa kosa la kutoa lugha ya matusi hivi
karibuni anatarajiwa kupandishwa tena kwenye mahakama hiyo kwa tuhuma ya
kushiriki kuchoma moto basi la Mtei lililogongwa pikipiki iliyokuwa
inatumiwa na watu wanne wa familia moja kwenda shambani.Wanafamilia
watatu,walipoteza maisha papo hapo.
Baadhi
ya lugha ya matusi inayodaiwa kutolewa na diwani huyo,ni “nyinyi wasege
tu,wapumbavu,hamna akili,vibaraka wa Mtei,mnakamata watu ovyo vyo mna
njaa mnataka kuchukua shilingi elfu kumi kumi kwa wapiga kura wangu”.
Mwendesha
mashitaka Chemu Mussa,alidai mbele ya hakimu Aisha Mwetindwa kuwa mnamo
januari 12 mwaka huu saa 1.30 asubuhi huko katika kijiji cha Ijanuka
kata ya Unyambwa tarafa ya Mungumaji manispaa ya Singida,mshitakiwa
Shaban aliwatolea lugha ya matusi maafisa wa polisi kitendo
kilichoelekea kusababisha kutoweka/kuvunjika kwa amani.
Amesema
tukio hilo lilitokea wakati maafisa hao wa polisi walikuwa kazini
wakilinda amani na utulivu kwenye eneo ambalo wananchi wa kata ya
Unyambwa walichoma basi la kampuni ya Mtei.
Mshitakiwa amekana shitaka na yupo nje kwa dhamana ya shilingi laki tano had februari 25 mwaka huu,kesi yake itakapotajwa tena.
Wakati huo huo,Jamhuri inatarajia kuita mashahidi sita kutoa ushahidi dhidi ya mshitakiwa diwani Satu.
Mashahidi hao ni D/ssge Mohammed,F531 D/C Boniface,A/INSP.Hassan,D.9749,D/CPL.Ally,G.6041 D/C Sikitu na E.4998.D/CPL.Mohammed.
0 comments:
Post a Comment