MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Friday, 28 February 2014

KUMBUKA LEO UWANJA WA TAIFA: (MTOTO HALALI NA HELA) NI MOTO YANGA v AL AHLY!!

 
YANGA_v_ALAHLYMABINGWA WA TANZANIA BARA, Yanga, Leo hii wanatinga Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kuwavaa Mabingwa wa Afrika, Al Ahly, katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Kwanza ya CAF CHAMPIONZ LIGI.
Timu hizi zitarudiana huko Cairo, Misri hapo Machi 9.
Wakati Al Ahly ikiwania kutwaa Ubingwa wao wa 3 mfululizo wa Afrika na ambao utakuwa Ubingwa wao 9, Yanga bado hawajaambua kitu kwenye michuano hii mikubwa Barani Afrika.
Wakati Yanga ipo Nafasi ya Pili kwenye VPL, Ligi Kuu Vodacom, na imepitwa tu na Azam FC kwa vile wamecheza Mechi moja zaidi, Al Ahly, wanaotetea Ubingwa wao wa Misri waliotwaa Mwaka 2011 kwani 2012 Ligi haikuchezwa huko Misri kutokana na vurugu, Msimu huu wapo Nafasi ya 4 baada kufungwa Mechi 3 katika Mechi 9 za Ligi.
Ingawa Al Ahly ni miamba wa kweli wa Afrika, Kihistoria mbinu zao za kucheza Ugenini ni kujihami na kuhakikisha hawafungwi ili ‘waue’ huko Cairo.
Hivyo Mechi hii ya Leo ni wazi mzigo mkubwa utakuwa kwa Washambuliaji wa Yanga wakiongozwa na Supastraika Mrisho Ngassa, ambae alipiga Hetitriki mbili katika Mechi mbili za Raundi iliyopitwa walipoitwanga Komorozine ya Comoro Jumla ya Bao 12-2, pamoja na wenzake Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza na Emmanuel Okwi.
Ngome ya Al Ahly, chini ya Mkongwe Wael Gomaa, ni imara na wana Wachezaji hatari kina Gedo na Emad Meteb lakini safari hii watamkosa Gwiji Mohammed AbouTrika ambae amestaafu.
VIKOSI VINAWEZA KUWA:
YANGA: Juma Kaseja, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub,  Kelvin Yondani,  Frank Domayo, Saimon Msuva, Mrisho Ngasa, Didier Kavumbagu, Emmanuel Okwi, Hamis Kizza
AL AHLY: Sherif Ekramy, R. Rabia, S. Samir, Wael Goma, S. Moawad, H. Ashour, S. Ahmed, A. Saied, A. Shoukri, R. Sobhi, A. Raouf
REFA: Haileyesus BAZEZEW BAZEZEW BELETE [Ethiopia]
CAF CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Kwanza
Jumamosi Machi 1
Dynamos – Zimbabwe v AS Vita Club - Congo, DR
Young Africans – Tanzania v Al Ahly - Egypt
AC Leopards de Dolisie – Congo v Primeiro de Agosto - Angola
Flambeau de l’Est – Burundi v Coton Sport FC - Cameroon
Nkana FC – Zambia v Kampala City Council FC - Uganda
Gor Mahia – Kenya v Espérance Sportive de Tunis - Tunisia
Al Zamalek – Egypt v Kabuscorp - Angola
Kaizer Chiefs - South Africa v Liga Muculmana de Maputo – Mozambique
Stade Malien de Bamako – Mali v  Al-Hilal - Sudan
Jumamosi Machi 2
Enyimba International FC – Nigeria v AS Bamako - Mali
Entente Sportive de Sétif - Algeria v ASFA-Yennenga - Burkina Faso
Berekum Chelsea – Ghana v Al Ahli - Benghazi - Libya
Les Astres de Douala - Cameroon v TP Mazembe - Congo, DR
The Barrack Y.C.II – Liberia v Sewe Sport - Ivory Coast
Horoya Athlétique Club – Guinea v Raja Club Athletic - Morocco

RAISI KIKWETE AZINDUA BUNGE LA KATIBA MPYA WIKI IJAYO

 
Jakaya-Kikwete1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Ijumaa, Februari 28, 2014 hatahutubia taifa katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi kama ilivyo kawaida.
Hotuba hiyo haitakuwepo kwa sababu awali Rais Kikwete alitarajiwa kuzindua Bunge Maalum la Katiba kwa hotuba rasmi Bungeni mjini Dodoma leo kabla ya ratiba ya shughuli za Bunge hili kufanyiwa mabadiliko. Rais Kikwete sasa atalizindua Bunge hilo wiki ijayo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

AFISA MSTAAFU WA NMB AFARIKA DUNIA KWENYE AJALI YA BASI NA TRENI

 
DSC06845
Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Manyoni, Dk.Kitundu Jackson ,akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya mapokezi ya majeruhi wa basi la bunda lililogonga kichwa cha Treni leo.Picha zote na Nathaniel Limu.
DSC06809
Bbasi la Bunda lililokuwa likitokea mjini Dodoma linakwenda jijini Mwanza na kugonga kichwa cha Treni maeneo ya mjini Mnayoni,linavyoonekana katika picha baada ya kugonga.
DSC06818
Baadhi ya majeruhi wa basi la Bunda lililogonga kichwa cha Treni mjini Manyoni,wakiwa wanapatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Manyoni.
DSC06819
Na Nathaniel Limu, Manyoni
AFISA Mstaafu wa NMB benki tawi la Manyoni mkoani Singida ambaye kwa sasa alikuwa Mhasibu wa SACCOS ya chama cha walimu Tanzania Manyoni,Belida Kombo amefariki dunia baada ya basi la kampuni ya Bunda alilokuwa akisafiria kugonga kichwa cha treni  na kujeruhi abiria wengine 39.
Basi hilo T.782 BKZ aina ya scania lililokuwa Farak Adamu lilikluwa likitokea Dodoma mjini kuelekea jijini Mwanza,liligonga kichwa cha treni eneo la makutano ya barabara kuu ya Dodoma – Singida na reli eno  la round about ya Manyoni mjini leo saa moja na nusu asubuhi.
Bi Kombo ambaye alipandia  basi hilo katika kituo cha mabasi cha Manyoni mjini na alifariki dunia dakika chake wakati akihangaika kutafuta kiti.Pia ndugu zake waliomsindikiza wakiwa bado hawajaondoka eneo lam kituo cha mabasi.
Akizungumza na waandishi wa habari Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Manyoni,Dk.Kitundu Jackson amekiri kwamba amepokea majeruhi 39 wa ajali ya treni na basi na kati yao sita wana hali mbaya.
 Amesema majeruhi walio na hali mbaya ni pamoja na kondakta wa basi Masage Bunyema na kwamba baadhi watapewa rufaa ya kupelekwa hospitali ya mkoa wa Dodoma na wengine katika hospitali ya misheni ya St.Gasper Itigi.
 “Tayari majeruhi wawili tumeisha wapa rufaa kwenda kupata matibabu katika hospitali ya mkoa ya Dodoma mjini na sista mmoja tumempeleka katika hospitali ya misheni ya St.Gasper Itigi”,alifafanua zaidi Dk.Kitundu.
 Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Manyoni,Fatma Toufiq ameiangiza mamlaka ya TRL na TANROADS kujenga haraka kuweka mtumishi  wa kutoa angalizo kwa vitambaa juu ya gari la moshi linapopita katika eneo hilo ambali kumetokea ajali tatu katika kipindi kifupi kilichopita.
Aidha,mashuhuda wa ajali hilo,wamedai kuwa hicho kichwa cha treni kilichokuwa kikitokea katika kijiji cha Aghondi,dereva wake alijitahidi kupiga honi kali ili kumwonya dereva wa bunda basi lakini dereva huyo hakujali.Kama haitoshi,dereva wa hiece aliyekuwa apishane na basi hilo,alimumulika kwa taa akimwonya asimame ili kipisha kichwa hicho,lakini hakujali pia.
Watu hao wamedai kuwa dereva wa basi hilo alikuwa kwenye mwendo kasi wakati akipewa onyo hilo la kupisha kichwa cha treni lipite.

TAARIFA KUHUSU HOTUBA YA RAISI YAMWISHO WA FEBRUARI 2014


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Ijumaa, Februari 28, 2014 hatahutubia taifa katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi kama ilivyo kawaida.

Hotuba hiyo haitakuwepo kwa sababu awali Rais Kikwete alitarajiwa kuzindua Bunge Maalum la Katiba kwa hotuba rasmi Bungeni mjini Dodoma leo kabla ya ratiba ya shughuli za Bunge hili kufanyiwa mabadiliko. Rais Kikwete sasa atalizindua Bunge hilo wiki ijayo.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.

Dar es Salaam.


28 Februari, 2014
 

UMOJA WA MATAIFA WAZINDUA KUMBUKUMBU ZA MAUWAJI YA RWANDA


tutu_cf5cb.jpg
Mmoja wa manusura wa mauaji ya maangamizi ya Rwanda ya mwaka 1994 akíwaombea wahanga wa mauaji mbele ya mafuvu yao katika kaburi la pamoja la Nyamata.
Umoja wa Mataifa umewasha mwenge kuzindua mkururo wa matukio yaliyopangwa kufanyika kwa nia ya kukumbuka miaka 20 ya mauaji ya maangamizi ya mwaka 1994 nchini Rwanda ambapo zaidi ya watu 800,000 waliuawa.
Akizungumza jijini New York katika kile kilichopewa jina la "Kwibuka 20", Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, alisema miaka 20 baada ya mauaji hayo ya maangamizi, kushindwa kwa jumuiya ya kimataifa kuzuia maafa nchini Syria ni jambo la aibu. Idadi ya washaopoteza maisha hadi sasa nchini Syria ni 140,000 kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Hata hivyo, Ban Ki-moon ameusifu uwezo wa Rwanda kuungana na kupatanisha baada ya mkasa huo na kusema umekuwa kivutio. Mauaji ya Rwanda yalianza masaa machache baada ya ndege iliyokuwa imembeba Rais Juvenal Habyarimana kuangushwa wakati ikikaribia mji mkuu, Kigali, tarehe 6 Aprili 1994.
Ndani ya siku 100 baada ya hapo, mauaji dhidi ya jamii ya Kitusti na Wahutu wenye msimamo wa wastani yaliangamiza roho za watu wapatao laki nane.
Wakati huo Umoja wa Mataifa ulikuwa na kikosi kidogo cha walinda amani nchini Rwanda, lakini Baraza la Usalama lilikataa kuongeza askari zaidi kukabiliana na mauaji hayo ya maangamizi, na hata nchi moja moja hazikutoa msaada wowote.
Syria kama Rwanda?
Hali inaonekana kufanana na hiyo kwa mauaji ya Syria, ambako hadi sasa bado Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limegawika vibaya juu ya mgogoro huo, ingawa Jumamosi iliyopita lilikubaliana kwa kauli moja juu ya azimio linaloyaruhusu mashirika ya misaada kuingia kwenye maeneo mbalimbali nchini humo.
Katika halfa hiyo ya hapo jana, Ban Ki-moon alisema licha ya Umoja huo kujifunza namna ya kuzuia maafa kama ya Rwanda, lakini hakuna uhakika kwamba matukio kama hayo hayawezi kujirejea.
"Mauaji ya maangamizi nchini Rwanda yalikuwa ni ishara kubwa ya kushindwa kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua dhidi ya uhalifu mbaya kabisa. Tunajua vyema zaidi sasa kuliko hapo kabla kwamba mauaji ya maangamizi si tukio moja tu, bali mchakato unaojumuisha mambo kadhaa na muda mrefu." Alisema Ban Ki-moon.
Ulaya nako kwatajwa
Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alizungumzia pia kupanda kwa kiwango cha chuki dhidi ya wahamiaji, Waislamu na jamii ya Waroma barani Ulaya na pia uvunjwaji mbaya kabisa wa haki za binaadamu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Umoja wa Mataifa unajaribu sasa kukabiliana na mauaji yanayochochewa kidini kwenye Jamhuri hiyo ya Afrika ya Kati, lakini hali inatajwa kuwa mbaya.
Wiki iliyopita, Ban Ki-moon alitoa wito wa kutumwa haraka kwa wanajeshi na polisi 3,000 ili kusaidiana na walinda amani 6,000 kutoka Umoja wa Afrika. Tayari wanajeshi 1,6000 wa Ufaransa wako huko, na Umoja wa Ulaya umeahidi kutuma wengine 500.
Chanzo, dw.de/swahili  

MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA ODM WAANZA NCHNI KENYA



ODINGA_a3464.jpg
Raila Odinga kiongozi wa chama cha ODM nchini Kenya.
Chama cha siasa nchini Kenya, ODM, jana kikianza mkutano wake mkuu wa siku mbili ambao pamoja na mambo mengine utafanikisha kupatikana kwa safu mpya ya uongozi wa chama hicho baada ya uchaguzi wa leo.
Mkutano huo uliwakutanisha viongozi na wanachama wa chama hicho kutoka maeneo mbalimbali ya taifa hilo. Hamisi Rachuri niongozi wa vijana wa ODM jimbo la Kwale na Sudi Mnette kwanza alitaka kujua matumaini yake katika mkutano huu.Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Chanzo, dw.de/Swahili

WANAMGAMBO WA NIGERIA WAUWA WATU 33

NIGERIA_5e951.jpg
Mabaki ya chuo cha serikali ambapo wanafunzi 60 walichomwa moto hadi kufa Februari 25, 2014
Shambulizi hilo la Alhamis karibu na mpaka wa Cameroon lilifanyika siku moja baada ya mashahidi kuripoti kuwa takribanu wanafunzi 60 waliuwawa katika chuo cha serikali.
Mashahidi na maafisa wa ndani kaskazini mashariki mwa Nigeria wanasema kundi linalotuhumiwa la wanamgambo wa Boko Haram limeuwa watu 33 na kushambulia kwa bomu chuo cha kidini katika jimbo la Adamawa.
Jeshi ambalo mara nyingi haliamini taarifa za idadi ya vifo kutoka kwa mashahidi limesema washambuliaji sita waliuwawa katika tukio hilo pamoja na mwanajeshi mmoja na raia watatu .
Shambulizi hilo la Alhamis karibu na mpaka wa Cameroon lilifanyika siku moja baada ya mashahidi kuripoti kuwa karibu wanafunzi 60 waliuwawa katika chuo cha serikali karibu na jimbo hilo la Adamawa.
Chanzo, voaswahili

HII NDIO ADHABU ALIYO PEWA KOCHA WA MAN CITY PELLEGRINI NA UEFA

PELLEGRINI_a9740.jpg

Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini.

Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini amepigwa marufuku mechi mbili na UEFA asisogelee eneo la kiufundi la uwanja kwa kumlaumu mwaamuzi baada ya klabu yake kushindwa na Barcelona katika michuano ya klabu bingwa ya Ulaya.
Pellegrini alisema baada ya timu yake kushindwa 2-0 nyumbani kwamba mwaamuzi kutoka Sweden Jonas Eriksson "hakua mwaadilifu kwa timu zote mbili".
Alituhumiwa kwa ukosefu wa nidhamu na amepewa adhabu ya kukaa jukwaani pamoja na mashabiki katika mkondo wa pili wa mchuano na Barcelona mnamo Machi 12 March, poja na Mechi nyingine za ziada.
Adhabu ya mechi moja nyingine imesimamishwa kwa miaka miwili.
Chanzo, bbcswahili

YANGA: YAZIDI KUJIGAMBA AL-AHLY LEO MKIINGIA TU! TUNAWACHINJA

 
WIKIENDI hii zinachezwa mechi 16 za raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Lakini macho ya Afrika nzima yapo Dar es Salaam ambapo mabingwa watetezi wa mashindano hayo, Al Ahly, itacheza na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa.
Afrika inafuatilia kwa karibu mechi hiyo kutokana na kupepesuka kwa Ahly kwenye ligi yao ya ndani katika siku za hivi karibuni huku Yanga ikionekana kupania kuangusha mbuyu uliowashinda Waafrika wengi.
Yanga imesisitiza kwamba itapambana kwa namna yoyote ile kuhakikisha inaidhalilisha Al Ahly jijini Dar es Salaam na kurahisisha kazi ya mchezo ujao ambao utakuwa ugenini Cairo.
Si wachezaji tu, hata kocha Hans Pluijm amepania kuweka historia ya aina yake akiwa na Yanga kwani ana uzoefu mkubwa na mashindano hayo. Mechi hiyo itakayoanza saa 10:00 jioni, itashuhudia ushindani wa aina yake huku Yanga ikipania kushambulia kwa nguvu na kubana sehemu ya kiungo na beki.
Yanga kabla ya kufika katika mchezo huo utakaochezeshwa na mwamuzi kutoka Ethiopia, Bazezew Belete, iliiondoa Komorozine ya Comoro kwa mabao 12-2. Yanga imekuwa ikijinoa kwenye Uwanja wa Boko Beach Veteran ulioko Tegeta, nje kidogo ya jiji huku ikipiga kambi kwenye hoteli ya Bahari Beach.
Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara wamekuwa wakipiga tizi asubuhi na jioni huku kocha akisisitiza zaidi umakini na kutumia nafasi pamoja na kuwajenga kisaikolojia wachezaji wake.
Kwa mujibu wa mazoezi yake, Yanga huenda ikaanzisha kikosi hiki; Deo Munishi 'Dida'/Juma Kaseja, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondani, Frank Domayo, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Mrisho Ngassa, Emmanuel Okwi na Hamis Kiiza. Katika nafasi ya kipa, Dida, ameonekana kuwa chaguo la kocha, lakini Juma Kaseja pia ana nafasi ya kuanza.
Okwi atashuka uwanjani kuichezea Yanga kimataifa kwa mara ya kwanza baada ya Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) kubariki usajili wake Jangwani.
Yanga huenda ikatumia mifumo miwili ya 4-3-3 na 4-3-2-1 ambayo hutumiwa pia na Ahly ambayo huenda ikajilinda zaidi.
Pluijm aliishusha Yanga mazoezini kwenye Uwanja wa Taifa jana Ijumaa jioni na baadaye wakafanya wapinzani wao.
"Hatuwezi kuwaogopa kabisa Ahly, nafurahi kuona kila kitu kipo sawa morali kwa wachezaji iko juu kwa kiwango cha kutosha, tutawashangaza wote wanaotubeza wakifikiri Yanga ni timu ndogo. Lakini tunawaheshimu Ahly kupitia rekodi yao katika mashindano haya," alisema kocha huyo.
Wachezaji wa Yanga wameshatangaziwa zaidi ya Sh100 milioni na matajiri wa timu hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Kimataifa, Seif Ahmed 'Seif Magari' na Makamu wake, Mussa Katabaro na Abdallah Bin Kleb, ambao wamepania kuweka historia katika uongozi wao chini ya Yusuf Manji.
Ahly tayari imepatwa na wasiwasi kwani juzi Alhamisi iliwatimua madereva wa magari waliyoyakodi wasishuhudie mazoezi yao kwa hofu ya kufanyiwa mizengwe. Pia katika hoteli ya Hyat Kempinski walipofikia, Waarabu hao wanafanya mambo kwa machale.
Yanga inatakiwa kuwa makini na washambuliaji wa Ahly, Mohamed Nagy 'Gedo' anayevaa jezi namba 15 na Amri Gamal wa jezi namba 17, ambao hawana masihara katika eneo la hatari kwa umahiri wao katika umaliziaji wa pasi za mwisho, hivyo ni wazi Cannavaro na Yondani wanatakiwa kuhakikisha wanawanyima nafasi ya kusogea karibu na eneo la 18. Lakini pia kuhakikisha hawaruki peke yao kutokana na shabaha ya vichwa vyao.
Ahly ni hatari kwa mashambulizi ya kutoka katikati ya uwanja, lakini pia hata mawinga wake hasa wa kulia huzalisha mabao yao.
Wakati akitua Jumatano kocha wa Ahly, Mohamed Youssef, alisema: "Tunawaheshimu Yanga, ni moja ya timu bora Tanzania kama ilivyo Simba. Lakini tumejiandaa vizuri kabla ya mechi hii, tunataka kuwaondoa ili tuendelee na mashindano haya, tunataka kupata ushindi hakuna shida katika hilo."
Minziro aonya mabeki
Kocha Msaidizi wa zamani wa Yanga ambaye sasa anainoa JKT Ruvu, Fred Minziro, ameonya kuwa mabeki wanapaswa kuacha uzembe na kufanya kazi ya ziada.
Minziro aliyekuwa akiifundisha Yanga kwenye mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara, alisema: "Yanga wana washambuliaji wakali, tatizo lipo kwa mabeki ambao mara nyingi huwa wanaigharimu timu kwa makosa ya kizembe.
"Kama watatumika akina Cannavaro, Kevin Yondani, Mbuyu (Twite) na Oscar (Joshua) basi wapangiwe majukumu maalumu wasiingiliane. Beki ya Yanga inahitaji kuwa na mawasiliano mazuri na kipa, wasimpoteze kipa na kumfanya abebeshwe lawama."
Kibadeni atoa ufundi
Kocha mkongwe wa Ashanti United, Abdallah Kibadeni, amemwambia Mholanzi, Hans Pluijm na wachezaji wake kuwa kama wanataka kusonga mbele kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika basi wasiruhusu bao nyumbani.
"Ninawashauri Yanga kushambulia goli la wapinzani wao dakika zote 90 na siyo kulinda goli lao, kikubwa wanachotakiwa ni kujiamini na kutoihofia Al Ahly. Kweli wapinzani wao ni timu bora, lakini ninaamini Yanga nao wapo vizuri wana washambuliaji wenye uwezo mkubwa," alisema Kibadeni.
Logarusic aipa mbinu
Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic, amewataka Watanzania wote wakiwamo wa timu yake, kuishangilia Yanga dhidi ya Al Ahly bila kujali itikadi zao za kisoka, lakini akaipa onyo klabu hiyo ya Jangwani kwamba isiidharau mechi hiyo.
"Yanga ina nafasi kubwa ya kushinda kwani imetoka kupata matokeo mazuri katika ligi yetu, timu za Kiarabu sasa zinaweza kuwa sawa na za Afrika Mashariki kwani uwekezaji wa soka umekua mkubwa kama Afrika Kaskazini na Magharibi," alisema.
"Yanga wacheze kwa kujiamini na kutodharau hata nafasi moja wanayopata, ni vyema wakashinda kama bao 1-0 au 2-0, wasiruhusu bao kwani faida ya bao la ugenini kwa Ahly inaweza kuwaweka mahali pabaya, wawachunge mawinga wa jamaa, maana ni hatari na wanajua wanachofanya."
Chanzo:Mwanaspoti

KUMBE MWALIMU NYERERE ALITAKA SERIKALI TATU ?


    nyerere_bc9a8.png
    Na Fredy Azzah, Mwananchi
    Dar es Salaam. Wakati mjadala wa Katiba Mpya hususani muundo wa Muungano ukipamba moto, imebainika kuwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kupendekeza kuanzishwa Serikali ya Tanganyika, kama sharti la kuingia kwenye Shirikisho la Afrika Mashariki.
    Maelezo hayo ya Mwalimu Nyerere yapo kwenye kitabu chake cha Uongozi Wetu Na Hatima ya Tanzania kilichoandikwa mwaka 1994 na kutolewa 1995
    .
    "Wakati Mwalimu anaandika kitabu hiki mwaka 1994 taifa letu lilikuwa linakabiliwa na changamoto kadhaa za kihistoria ambazo ndizo zilimfanya kuingilia kati na kuandika kijitabu hiki ambacho kilikuwa kama nasaha, onyo, na usia kwa Watanzania," inasema sehemu ya utangulizi wa kitabu hicho.
    Katika sura ya nne ya kitabu hicho, pamoja na mambo mengine Mwalimu Nyerere alizungumzia suala la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo alieleza sababu zilizofanya muungano wa serikali mbili ukaanzishwa.
    "Labda ni vizuri kukumbuka kwamba shabaha ya baadhi yetu ilikuwa ni kuziunganisha nchi za Afrika Mashariki ziwe nchi moja," alisema katika kitabu chake hicho.
    Alieleza kuwa, wakati Zanzibar na Tanganyika zinaungana, Kenya, Uganda na Tanganyika zilikuwa katika mazungumzo ya kutafuta uwezekano wa kuungana.
    "Kama jambo hilo lingetokea, nina hakika kabisa kwamba mfumo wa nchi mpya ambayo ingezaliwa ungekuwa ni wa shirikisho; ama shirikisho la nchi tatu zenye serikali nne, au shirikisho la nchi nne zenye serikali tano.
    "Kwa kweli hata kesho nchi za Afrika Mashariki zikiamua kuungana na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye serikali mbili ya Zanzibar na ya Tanganyika kuliko Tanzania yenye serikali mbili, ya Tanzania na Zanzibar," alisema.
    Alisema kwa kufanya hivyo, wapendao Utanganyika watakuwa wazalendo zaidi, badala ya kuwa wasaliti, wakiazimia Afrika ya Mashariki iliyoungana kuwa nchi moja, kuliko Tanzania iliyotengana ikawa nchi mbili.
    Baadhi ya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wakizungumzia suala hilo, walisema kuwa ni vyema kuangalia zaidi matakwa ya wananchi kuliko kujali tu mfumo.
    Mmoja wa wahadhiri hao, Faraja Christoms alisema wakati Mwalimu Nyerere akiandika kitabu cha Uongozi Wetu Na Hatima ya Tanzania, alikuwa na hofu ya kumeguka kwa muungano.
    "Wakati ule kulikuwa na wale wabunge wa G55 jina walilobatizwa na Profesa Issa Shivji, hawa wabunge walikuwa wanaona kama Zanzibar inapendelewa sana, walikuwa wanaona kama wanalalamika tu kama watoto
    "Lakini ukiwasikiliza na wenyewe Wazanzibari walikuwa na hoja, waliona kama Serikali ya Muungano ndiyo imekuwa ya Tanganyika kwa hiyo vitu vya Muungano vilikuwa vinainufaisha zaidi Tanganyika," alisema.
    Alisema kutokana na hali hiyo ndiyo Mwalimu Nyerere alipoamua kuandika kitabu hicho.
    Christoms alisema kwa mfumo wa sasa ulivyo ni vyema maoni ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba yakaheshimiwa, kwani hayatofautiani sana na yale ya tume nyingine zilizowahi kuundwa kuangalia suala la Muungano.
    Alisema kwa kuwa tayari Zanzibar ina katiba yake ambayo imetambua visiwa hivyo kama nchi, siyo rahisi kubadilisha hali hiyo.
    "Ukisema tuendelee na serikali mbili, kero za Wazanzibari hazitatatulika, ukitaka kulitatua hili kwanza useme haya mambo yasiyo ya Muungano nani ayashughulikie na yale ya Tanganyika pia yatashughulikiwa na nani?
    "Mimi mwenyewe sioni kwa nini watu waseme tukiwa na serikali tatu muungano utavunjika kwa sababu muungano ni ridhaa ya watu, kwa sababu tayari Zanzibar ilishasema kuwa yenyewe ni nchi, Tume ya Warioba imebeba mawazo ya watu kwa hiyo ni vyema tukayaheshimu," alisema Christoms.
    Kwa upande wake Dk Aldin Mutembi alisema, "Mimi sijaingia ndani sana kwenye suala la serikali tatu ama mbili, lakini naungana na maoni ya Tume ya Warioba."
    Tume ya Warioba ilipendekeza kuwapo kwa serikali tatu.
    Mhadhiri wa Chuo cha Diplomasia, Dk Wetengere Kitojo alisema kuwa, mawazo ya mwalimu yalikuwa serikali mbili kwa kuwa lengo lilikuwa katika kuelekea kwenye muungano wa serikali moja.
    Alisema kwa sasa baadhi ya watu wanapiga kelele kutaka uwepo wa serikali mbili na wengine serikali tatu, ingawa ndani yake wapo ambao hawautaki kabisa muungano.
    "Serikali mbili ni muungano bora zaidi, tumekuwa na mfumo huu kwa muda mrefu, lakini hatuoni kama kuna mwelekeo wa serikali moja, ndiyo maana watu wengine wameona bora tuwe na serikali tatu ili tupunguze kero ambazo zimeshindwa kutatuliwa kwa muda mrefu ndani ya mfumo wa serikali mbili.
    "Mimi naona cha msingi ni nia ya dhati, wapo wanaotaka serikali mbili lakini hawana nia ya dhati ya muungano, wapo wengine serikali tatu lakini pia hawautaki muungano. Lengo ni muungano kamili, serikali tatu ni kurudi nyuma, ila sasa kama kwa miaka yote tumeshindwa kufikia lengo la serikali moja wengine wanaona bora turudi kwenye serikali tatu
    Alisema kuwa, kwa mtazamo wake serikali mbili ni bora zaidi ili baadaye iwepo moja lakini kama suala hilo limeshindikana ni bora kuwepo na mfumo wa serikali tatu.
    Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Emanuel Muya alisema mazingira yaliyomfanya Mwalimu Nyerere kuandika kitabu cha Uongozi Wetu Na Hatima ya Tanzania, ni tofauti na haya yaliyopo leo.
    "Pamoja na yote bado kuna umuhimu wa kuungana Tanganyika na Zanzibar, hakuna anayetaka kuuvunja muungano, hata mwalimu alikuwa anataka muungano imara, alivyoondoka muungano ulikuwa imara.
    "Uwe unakubalika pande zote, kwa sasa una matatizo pande zote, lazima tukubali kupata mazingira aliyokuwa akiyataka Mwalimu," alisema.

    BENKI YA DUNIA YAKEMEA UHARIBIFU WA CHAKULA

    BBC_7e624.jpg
    Basi Ripoti mpya kutoka benki ya dunia inasema kuwa robo ya chakula chote kinachokuzwa duniani hupotea ama kutupwa, na sasa inawataka raia kufikiri kwa makini kile kuhusu uharibifu huu wa chakula.
    Inasema kuwa katika maeneo kama vile Marekani na Uchina ,watumiaji wa chakula ndio wa kulaumiwa pakubwa kwa kupoteza chakula hicho.
    Lakini katika jangwa la Sahara chakula kingi hupotea wakati wa uzalishaji.
    Benki ya dunia inasema kuwa kati ya asilimia 25 na 35 ya chakula chote kinachokuzwa duniani hutupwa.
    katika mataifa yanye utajiri wa viwanda ,lawama kubwa zaidi huwaendea watumiaji wa chakula hicho ambao hukiwacha chakula kuoza katika jokovu.
    Raia wa marekani kazkazini ni miongoni mwa wale walio na lawama kubwa kwa kuwa asilimia 61 ya chakula chao huharibika wakati wa matumizi.
    Mwandishi wa ripoti hiyo Jose Cuesta anasema kuwa kile kinachohitajika ni kubadili tamaduni.
    Lakini katika jangwa la Sahara chakula kingi huharibika wakati wa uzalishaji .
    Benki kuu duniani inasema kuwa kiwango cha chakula kinachotupwa kinaweza kutofautisha kati ya chakula bora na uhaba wa chakula katika mataifa mengi.
    Imeonya kuwa iwapo mbinu za uzalishaji hazitaimarishwa na tabia za kula kubadilishwa ,dunia huenda ikakumbwa na uhaba wa chakula kwa idadi kuu ya watu inayozidi kuongezeka.
    Chanzo, bbcswahili

    TFF YAITAKIA HERI YANGA MTANANGE AFRIKA NA AL -AHLY!

    >>YANGA v AL AHLY: MAANDALIZI YAKAMILIKA!
    >>VPL: MAREKEBISHO-PRISON, SIMBA KUCHEZA MACHI 9!
    >>TFF KUADHIMISHA MIAKA 50 KUJIUNGA FIFA, YAUNDA KAMATI!!
    SOMA ZAIDI:
    Release No. 035
    TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
    Februari 28, 2014
    YANGA_MJENGOMALINZI AUNDA KAMATI YA MIAKA 50 FIFA
    Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameunda kamati ya watu tisa kuratibu maadhimisho ya miaka 50 tangu TFF ilipojiunga na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
    TFF ilipata uanachama wa shirikisho hilo la kimataifa Oktoba 8, 1964 ambapo itaadhimisha miaka hiyo 50 kwa kufanya shughuli mbalimbali za mpira wa miguu.
    Kamati hiyo itaongozwa na Mhariri Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali, Gabriel Nderumaki wakati Katibu atakuwa Lina Kessy ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Wanawake (TWFA).
    Wajumbe ni Ahmed Mgoyi, Hoyce Temu, Teddy Mapunda, Ruge Mutahaba, Richard Kasesela, Boniface Wambura na Meneja Biashara wa TFF anayetarajiwa kuajiriwa hivi karibuni.
    Kamati itafanya kikao chake cha kwanza Jumatatu (Machi 3 mwaka huu) kwenye hoteli ya Courtyard iliyopo Upanda Seaview saa 7 mchana.
    KILA LA KHERI YANGA MECHI YA LIGI YA MABINGWA
    Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaitakia kila la kheri yake kwenye mechi yake ya kwanza ya raundi ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly kutoka Misri.
    Mechi hiyo inachezwa kesho (Machi 1 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia 10 kamili jioni. Timu hizo zitarudiana Machi 9 mwaka huu jijini Cairo, Misri.
    Maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika ambapo kamishna Abbas Sendyowa kutoka Uganda na waamuzi wanne kutoka Burundi tayari wapo nchini kwa ajili ya mechi hiyo inayotarajiwa kuvuta maelfu ya washabiki.
    Milango yote katika uwanja huo itakuwa wazi, ukiwemo ule wa upande wa Uwanja wa Ndani (Indoor Stadium) wakati Barabara ya Taifa (Taifa Road) itafungwa kuanzia chuo cha DUCE hadi msikitini kuanzia saa 4 asubuhi.
    Magari maalumu yenye sticker pekee ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani. Vilevile washabiki wanakumbushwa kuwa hawaruhusiwi kuingia uwanjani wakiwa na silaha au vifaa vyovyote vya chuma.
    MAREKEBISHO YA MECHI VPL, FDL
    Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya marekebisho madogo ya ratiba kwa mechi mbili za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na moja ya Ligi Daraja la Kwanza (VPL).
    Mechi namba 143 kati ya Tanzania Prisons na Simba iliyokuwa ichezwe Machi 8 mwaka huu sasa imesogezwa kwa siku moja hadi Machi 9 mwaka huu, kwa vile Machi 8 mwaka huu Mbeya City itautumia uwanja huo kwa mechi nyingine ya VPL.
    Nayo Mgambo Shooting iliyokuwa icheze na Kagera Sugar, Aprili 12 mwaka huu Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga sasa imesogezwa hadi Aprili 13 mwaka huu kwa vile Kituo cha Tanga kitakuwa na mechi mbili.
    Kwa upande wa FDL, mechi ya Mkamba Rangers na Kimondo SC sasa itachezwa Machi 3 mwaka huu badala ya Machi 9 mwaka huu mjini Ifakara. Mechi hiyo imerudishwa nyuma ili kuipunguzia gharama Kimondo SC kwani Machi 1 mwaka huu itacheza na Burkina Faso mjini Morogoro.
    Boniface Wambura Mgoyo
    Media and Communications Officer
    Tanzania Football Federation (TFF)

    LIGI KUU ENGLAND: CHELSEA KUBAKI KILELENI AU ARSENAL KUIPIKU?

    >>WENGER ASISITIZA LIGI KUU ENGLAND NDIO BORA!
    RATIBA MECHI ZIJAZO:
    [Saa za Bongo]
    Jumamosi Machi 1
    1800 Everton v West Ham
    1800 Fulham v Chelsea
    1800 Hull v Newcastle
    1800 Stoke v Arsenal
    2030 Southampton v Liverpool

    WENGER_BAADA_KUFUNGWAWAKATI Manchester City hawana Mechi ya Ligi Kuu England Wikiendi hii kwa vile Jumapili wako Uwanjani Wembley kucheza Fainali ya CAPITAL ONE CUP na Sunderland, Chelsea na Arsenal zina nafasi ya kujitanua kileleni kwa kuongeza pengo lao na City kuwa kubwa huku wao wenyewe wakigombea nani atakuwa Nambari Wani.
    Jumamosi, Vinara Chelsea, ambao wako Pointi 1 mbele ya Arsenal, watakuwa Ugenini kucheza na Fulham na Arsenal pia wapo Ugenini kuivaa Stoke City.
    Liverpool, ambao wako Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 1 nyuma ya Man City, wana nafasi nzuri ya kuipita City ikiwa nao pia watashinda Mechi yao ya Ugenini dhidi ya Southampton.
    Everton, ambao wako Nafasi ya 7, watakuwa Nyumbani Goodison Park kucheza West Ham na wakitoka Sare au kushinda wataishusha Man United ambao hawana Mechi Wikiendi hii.
    Mabingwa Watetezi Man United Mechi yao inayofuata ya Ligi ni Wikiendi ijayo hapo Machi 8 watakapokuwa Ugenini kucheza na West Bromwish Albion.
    WAKATI HUO HUO, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ameitetea Ligi Kuu England licha ya Vilabu vyake vinne kuanza vibaya kwenye Mechi za Kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UEFA CHAMPIONZ LIGI.
    Kwenye Mechi hizo, Arsenal na Man City zilichapwa 2-0 Nyumbani kwao walipocheza na Bayern Munich na Barcelona na Man United kufungwa 2-0 Ugenini na Olympiacos wakati Chelsea ilipata Sare ya 1-1 huko Uturuki dhidi ya Galatasaray.
    Hata hivyo, Wenger amedai Ligi Kuu England ipo kiwango cha juu na ametamka: “Ukweli Ligi hii ni ngumu Duniani kwani kiwango ni kizuri kuanzia Timu ya Kwanza hadi ya Ishirini. Ni Ligi pekee Ulaya ambayo ina hilo. Lazima ujue huko Ulaya Timu zote 4 za England zilifuzu toka Makundi yao. Baada ya Gemu moja huwezi ukaamua ubovu wao! Man City walicheza Mtu 10, Arsenal walicheza Mtu 10. Man City walicheza na Barcelona na Arsenal walicheza na Bayern Munich ambao ndio Mabingwa wa Dunia. Kucheza Mtu 10 ni ngumu! Baada ya hapo Timu nyingine mbili, Man United na Chelsea, bado wako kwenye nafasi kugeuza matokeo, wako Nyumbani!”
    Wenger alimaliza: “Ngoja tusubiri matokeo ya Mechi za pili kisha tuanze kusema mwelekeo wa Ligi hii, udhaifu au nguvu yake!”
    RATIBA:
    [Saa za Bongo]
    Jumapili Machi 2
    1930 Aston Villa v Norwich
    1930 Swansea v Crystal Palace
    1930 Tottenham v Cardiff
    MSIMAMO:
    NA
    TIMU
    P
    GD
    PTS
    1
    Chelsea
    27
    28
    60
    2
    Arsenal
    27
    25
    59
    3
    Man City
    26
    42
    57
    4
    Liverpool
    27
    35
    56
    5
    Tottenham
    27
    3
    50
    6
    Man United
    27
    12
    45
    7
    Everton
    26
    10
    45
    8
    Newcastle
    27
    -5
    40
    9
    Southampton
    27
    6
    39
    10
    West Ham
    27
    -3
    31
    11
    Hull
    27
    -2
    30
    12
    Swansea
    27
    -4
    28
    13
    Aston Villa
    27
    -10
    28
    14
    Norwich
    27
    -19
    28
    15
    Stoke
    27
    -15
    27
    16
    Crystal Palace
    26
    -18
    26
    17
    West Brom
    27
    -8
    25
    18
    Sunderland
    26
    -16
    24
    19
    Cardiff
    27
    -29
    22
    20
    Fulham
    27
    -32
    21
    RATIBA MECHI ZIJAZO:
    [Saa za Bongo]
    Jumamosi Machi 8
    1545 West Brom v Man United
    1800 Cardiff v Fulham
    1800 Crystal Palace v Southampton
    1800 Norwich v Stoke
    1800 West Ham v Hull
    2030 Chelsea v Tottenham

    BARABARA YA KIMARA HADI KIVUKONI KUKAMILIKA NDANI YA MIEZI SITA

     
    Picha 1
    Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (aliyekaa kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa Iyombe (katikati) pamoja na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale (aliyesimama) wakisafiri kwa basi kukagua utekelezaji wa ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam.
    Picha 2
    Mkurugenzi Mkuu wa DART Asteria Mlambo (kulia) akimwongoza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Said Meck Sadiki anayefuatana na Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kuegesha mabasi ya haraka kinachojengwa eneo la Jangwani, jijini Dar es Salaam.
    Picha 3
    Msimamizi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka kutoka TANROADS Mhandisi Barakaeli Mmari (aliyeshika kijiti) akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi kuhusu utekelezaji wa mradi wa mabasi yaendayo haraka katika eneo la Kimara jijini Dar es Salaam.
    Kampuni ya Strabag International GmbH inayotekeleza ujenzi wa barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi Kivukoni hapa jijini Dar es Salaam imetakiwa kuhakikisha kuwa  inakamilisha ujenzi wa sehemu hiyo ndani ya kipindi cha miezi sita ijayo kama mkataba wao unavyoelekeza.
    Waziri wa Ujenzi Mhe. Magufuli alitoa agizo hilo wakati akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara kwa ajili ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (Dar es Salaam Bus Rapid Transit – BRT) ambao umeelezewa kuwa na changamoto nyingi kiasi cha kusababisha usumbufu kwa watumia barabara hiyo kwa kipindi kirefu.
    Akimpatia taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale alimjulisha Waziri Magufuli kuwa kwa hivi sasa changamoto nyingi zimefanyiwakazi na mradi unaendelea kusimamiwa kwa karibu ili kuhakikisha kuwa hukuna ucheleweshaji zaidi katika hatua hii iliyobaki.
    Mkataba wa ujenzi wa barabara hizi pamoja na vituo vya mabasi ulisainiwa mwezi Desemba mwaka 2012 ukiwa umepangwa kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu kwa gharama ya Shilingi bilioni 280.
    Kwa upande mwingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Said Meck Saddik ambaye aliambatana na Waziri Magufuli katika ziara hiyo, amewataka wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zao ndani ya sehemu ambayo mkandarasi anaendelea na kazi waondoke kwani hiyo mbali ya kuwa kinyime na taratibu za uendeshaji biashara zilizowekwa lakini pia imekuwa ni moja ya kisingizio kinachotolewa kwamba uendeshaji wa shughuli hizo unachangia kuchelewa kukamilika kwa ujenzi huo.
    Waziri Magufuli akizungumza wakati wa kuhutimisha ziara hiyo, amemtaka mkandarasi kuhakikisha anaukamilisha mradi huo kwa muda na viwango vilivyokusudiwa. “Na kwa wale walio ndani ya eneo la ujenzi ni lazima sheria ichukue mkondo wake” alisisitiza Waziri Magufuli huku akimtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Kindondoni Mhandisi Mussa Natty kuhakikisha anasimamia zoezi hilo la kuondoa haraka wale wote wote walioingia katika eneo hilo la barabara kinyume na sheria.
    Aidha, Waziri Magufuli alielezea kushangazwa kwake kwa kuchelewa kuondolewa kwa nyaya za Tanesco katika maeneo ya City Squire na Morocco kwani fedha za kutekeleza kazi hiyo tayari zimelipwa muda kirefu. “Ucheleweshaji wa ainaa hii ndiyo unaotoa mwanya kwa mkandarasi kuanza kutoa visingizio vya kutokamilika kazi hii kwa wakati” ametahadharisha Mhe. Magufuli.
    Hata hivyo katika hatua nyingine Mhe. Magufuli amemtaka mkandarasi kuharakisha taratibu za kuifungua barabara  hiyo upande wa kuingia Dar es Salaam ambako kwa sasa hivi hakuna shughuli kubwa zinazofanyika ili kupungiuza adha ya msongamano wa magari yanayopishana katika njia moja ya upande wa kutokea mjini katika barabara hiyo ya Morogoro hasa kwa eneo kati ya Ubungo na Kiamara.
    Naye Msimamizi wa mradi huo kutoka TANROADS Mhandisi Barakaeli Mmari ameelezea kuwa, utekelezaji wa mradi huu wa usafiri wa haraka utajengwa katika awamu sita. Awamu ya kwanza ambayo ujenzi wake ndio huu unaoendelea inahusisha barabara zenye jumla ya kilometa 20.9 ambazo ni Kimara – Kivukoni, Magomeni – Morocco na Faya – Karikaoo. Hadi sasa mkandarasi amekwisha kamilisha asilimia 55 ya mradi wote.

    MTOTO ADOLOTEA NJAVIKE(1.4) ANAOMBA MSAADA WA MATIBABU KUTOKA KWA WASAMARIA WEMA

      ili aweze kufanyiwa upasuaji kutokana na Kichwa na Kiwiliwili kuungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi

    MTOTO Adolotea Njavike(1.4) ambae Kichwa na Kiwiliwili vimeungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.


    Mama Mkubwa wa Mtoto huyo, Salome Kiegu(35) mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Iyunga Jijini Mbeya anasema Mtoto huyo akiwa na mama yake walipata janga la moto katika mazingira ya kutatanisha waliangukia kwenye moto ambapo Mtoto huyo aliungua vibaya.


    Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu akiwa amempakata mtoto huyo

    Baadhi ya waandishi wa habari wakiongea na mama mkubwa wa mtoto huyo
    MTOTO Adolotea Njavike(1.4) anaomba msaada wa matibabu kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kufanyiwa upasuaji kutokana na Kichwa na Kiwiliwili kuungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.
    Akizungumza kwa masikitiko Mama Mkubwa wa Mtoto huyo, Salome Kiegu(35) mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Iyunga Jijini Mbeya anasema Mtoto huyo akiwa na mama yake walipata janga la moto katika mazingira ya kutatanisha waliangukia kwenye moto ambapo Mtoto huyo aliungua vibaya.
    Anasema tukio hilo lilitokea Mwaka jana Mwezi wa Nane lakini alipopatiwa matibabu katika kituo cha afya mtoto huyo aliungana ngozi ya kidevu na kifua hali inayomletea shida ya kula na kufurahi na wenzake.
    Anasema tangu kipindi hicho alimchukua mtoto huyo kwa mama yake na kuanza kuomba msaada wa matibabu baada ya kumpeleka katika Hospitali ya Ikonda iliyoko Makete Mkoani Njombe ambapo Wataalamu walimwambia atafute Shilingi Milioni Moja ili mtoto wake aweze kutibiwa.
    Ameongeza kuwa baada ya muda wataalamu hao walimwambia asubiri Wazungu kutoka Ulaya ambao wataweza kumtibia mwanaye ambapo baada ya kusubiri kwa muda kidogo Wazungu hao walifika na kumcheki Mwanaye kisha kumwambia wao hawana utaalamu isipokuwa aende CCBRT Dar Es Salaam ambako ataweza kutatuliwa tatizo lake.
    Aidha kutokana na kuambiwa hivyo Mama huyo anaomba msaada kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kumpeleka Mtoto wake kwa matibabu kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuweza kusafiri hadi DSM pamoja na gharama za matibabu kuwa kubwa.
    Amesema anahitaji zaidi ya shilingi Milioni 2 ili ziweze kumsaidia kusafiri kugharamia matibabu pamoja na huduma za Kawaida kipindi atakachokuwepo Jijini Dar Es Salaam wakati akisubiri matibabu ya Mwanaye.
    Mtu yeyote mwenye kuguswa na tatizo hilo anaweza kuwasiliana moja kwa moja na Mama huyo kupitia simu yake ya Mkononi namba 0752 986879 au Nyumbani kwake Iyunga Mtaa wa Maendeleo Jijini Mbeya.
    Na Mbeya yetu

    RAIS KIKWETE AKUTANA NA KATIBU MKUU WA EAC

     
    D92A0109 D92A0106 
    Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt.Richard Sezibera ikulu jijini Dar es Salaam leio asubuhi(picha na Freddy Maro)

    BALOZI WA FINLAND TANZANIA AKABIDHI VYETI KWA WAHITIMU WA MAFUNZO YA (TEHAMA) JIJINI DAR ES SALAAM

    001 (1) 
     Mkuu wa Idara Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano TTCL Bw, Adini Mgendi akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi,  Balozi wa Finland Tanzania, Sikka Antila,  wakati wa hafla ya kukabidhi Stashahada ya Udhamini katika Uongozi wa Tekenolojia ya Habari na mawasiliano (TEHAMA),kwa wahitimu wa mafunzo hayo (kulia), Mkuu wa Mafunzo Global e-Schools Community Inihative, Hellen Tapper (kushoto), Balozi wa Finland Tanzania Sikka Antila.Hafla hiyo ilifanyika katika Hotel ya New Afrika jijini Dar es Salaam Februari 27, 2014.002  
    Balozi wa Finland Tanzania,  Sikka Antila,  akisoma hotuba yake wakati wa  hafla ya kukabidhi Stashahada ya Udhamini katika Uongozi wa Tekenolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kulia Mkuu wa Idara Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano TTCL Bw, Adini Mgendi003  
    Balozi wa Finland Tanzania, Sikka Antila (kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Idara Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano TTCL Bw, Adini Mgendi cheti cha mafunzo hayo.004005 Baadhi ya waitimu wa mafuno ya stashahada ya udhamini katika uongozi wa Tekenolojia ya Habari na mawasiliano (TEHAMA) wakimsikiliza kwa umakini Balozi wa Finland Tanzania Sikka Antila akisoma hotuba yake.006 
    Balozi wa Finland Tanzania Sikka Antila akiwa kwenye picha ya pamoja na waitimu wa mafunzo hayo mara baada ya kuwakabidhi.
    PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA  DAR ES SALAAM