Monday, 2 December 2013

WACHEZAJI WA ERITRREA WATOWEKA KIMBINI

Uongozi wa soka nchini Kenya unasema kuwa wachezaji wawili wa timu ya soka ya Taifa la Eritriea wameondoka na hadi sasa hawajurudi kambini na haifahamiki waliko.

Afisa wa Kenya anayesimamia kikosi hicho Albert Shamola, alielezea kutoweka kwa wachezaji hao kambini: “Wachezaji wao wawili wametoweka na hawajulikani waliko baada ya mechi ya Ijumaa. Baada ya kipindi cha kwanza, baadhi yao walienda
kujisaidia na wakarejea kwa kipindi cha pili. Mchezo ulipomalizika na tukawa tunarejea kwenye basi ndipo tuligundua hawakuwepo,” amesema Shamola.

Afisa huyo alithibitisha kwamba wamelitaarifu Shirikisho la soka nchini na lile la CECAFA: “Tummelijulisha Shirikisho kuhusu tukio hilo na tayari wameanza kusakwa ila hadi kufikia sasa hamna bado hatujafanikiwa kuwapata,” akaongeza afisa huyo.

Huu ni mwaka wa tano kwa cha wachezaji wa timu hiyo kupotea wakitokea kwenye dimba la CECAFA. Mfano, mwaka 2012 walipotea wakati wa mashindano ya CECAFA yaliyoandaliwa jijini Kampala nchini Uganda, na mwaka 2011 walijificha wakati michuano hiyo jijini Dar es Salaam, Tanzania na baadaye kubainika kuwa walikuwa wanatafuta hifadhi ya kisiasa.

0 comments: