Saturday 1 June 2013

MWILI WA MSANII NGWEA KUWASILI KESHO JUMAPILI



MWILI wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, marehemu Albert Mangwea ‘Ngwair’ sasa unatarajiwa kuwasili nchini kesho badala ya leo kama ilivyotaarifiwa awali.M
 http://1.bp.blogspot.com/-6w6OrnTpMqY/UadLwEH2bXI/AAAAAAAACJE/Sj2S5Yk3YSM/s1600/579495_275410252604430_1485125168_n.jpg
Kwa mujibu wa taarifa ya kamati ya mipango ya mazishi ya msanii huyo iliyotolewa jana inayoongozwa na Kaka wa marehemu, Kenneth Mangwea, mwili huo utawasili Jumapili majira ya saa 8, mchana na kisha kufuata taratibu zingine.

“Mwili utafika nchini siku ya Jumapili majira ya saa nane mchana na sio Jumamosi (leo), kama ilivyotaarifiwa hapo awali,” ilieleza taarifa hiyo.

Sababu za mabadiliko hayo, imeelezwa ni kutokana na Watanzania waishio Afrika Kusini, kuomba kutoa heshima za mwisho, Jumapili.

Kwa hatua hiyo, kamati ilibainisha kuwa kwa wakazi wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani, watapata nafasi ya kuuaga mwili Jumatatu majira ya saa 2 asubuhi hadi 6 mchana na baada ya hapo, wataelekea Morogoro kwa ajili ya mazishi, Jumanne.

Aidha, kamati iliomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza, huku ikiomba wadau kuendelea kuwaombea kufanikisha salama shughuli hizo za mazishi

0 comments: