WADAU wa soka wamelitupia lawama Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) kuwa ni aibu
kwa chombo hicho kufuga madeni hadi mali zake kutaka kukamatwa.
Kauli za wadau
zimekuja siku moja baada ya Kampuni ya Udalali ya Flamingo Auction Mart kupewa
idhini na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kukamata magari mawili ya
shirikisho hilo
kufidia deni la sh mil. 51 zinazodaiwa na Safina Holding Campany.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti jana, Frederick Mwakalebela aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa
Shirikishio hilo, amelitupia lawama shirikisho hilo na Baraza la Vyama
vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) wenye mamlaka na michuano hiyo ya
Chalenji.
Hata hivyo,
Mwakalebela alielekeza lawama kwa Cecafa akisema wakiwa waandaaji wa michuano
hiyo, walipaswa kutoa sapoti kumaliza deni hilo badala ya kuwa mzigo kwa mwejeji, TFF.
Mwakalebela
alisema hata kama Cecafa wakishindwa kutoa sapoti, ni bora kwenye mgao wa
uwanjani likatolewa fungu kulipia madeni kama
hayo.
Naye Katibu
Mkuu wa Simba, Selestine Mwesigwa, akisema kitendo hicho ni aibu kwa shirikisho
hilo kwani
tahadhari ilipaswa kuchukuliwa kabla ya hali haijafikiwa hatua hiyo.
Alisema
inashangaza kuona deni hilo
linadumu kwa miaka mitatu pale michuano hiyo ilipofanyika chini ya udhamini wa
bia ya Tusker.
Mwesigwa
alisema ni aibu ya kujitakia kwa TFF na haitoi picha nzuri kwa klabu ambazo
ziko chini yake.
Aidha Mwesigwa
aliongeza kuwa ni wakati wa TFF kuwa makini katika mambo yake kwani ni muda
mrefu tangu kwisha kwa chalenji ya mwaka 2011.
Katibu Mkuu wa
TFF, Angetile Osiah, alisema jana deni hilo
lilitokana na gharana za malazi kwa waamuzi wa michuano ya chalenji.
0 comments:
Post a Comment