Thursday 20 June 2013

POLISI ATUHUMIWA KUUA MWANANCHI MKUTANONI (MBEYA)

Blogu ya Kalulunga inataarifu: POLISI ADAIWA KUUA RAIA MBOZI

TAARIFA kutoka eneo la njia panda Iyula wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya, zimesema kuwa barabara kuu ya Mbeya-Zambia imefungwa na wananchi baada ya mmoja wao kudaiwa kupigwa risasi na askari polisi.

Mwananchi aliyepo eneo la tukio amesema kuwa wananchi walikuwa kwenye mkutano nwa hadhara, ndipo wakajitokeza askari na kuzingira nyumba ya mwanakijiji mmoja aliyekuwa eneo la mkutano hali iliyomlazimu kuinuka na kwenda kuwauliza kulikoni ndipo ikazuka tafrani na kisha risasi zikaanza kurushwa na hatimaye mwananchi huyo kufariki.


Source:  Kalulunga blog

0 comments: