Friday, 7 June 2013

RAIS PUTIN WA URUSI ASEMA UKWELI KUA CHANA NA MKEWE



Tangazo la kuachana kwa Waziri Mkuu wa Urusi Vladimir Putin na mkewe baada ya ndoa iliyodumu kwa miaka 30 limeifadhaisha Urusi. 
 http://static.guim.co.uk/sys-images/Guardian/Pix/pictures/2013/6/6/1370546372828/Vladimir-and-Lyudmila-Put-010.jpg
Ndoa ya Putin na Lyudmila, mhudumu wa ndege wa zamani ambaye anajulikana kuwa ni mtu asiyependa kuonekana sana hadharani, yumkini ilikuwa tayari imekufa kwa miaka mingi ilikuwa mada ya uvumi miongoni mwa watu mashuhuri nchini Urusi na hata wananchi wa kawaida wa nchi hiyo. Lakini hatua ya Ikulu ya Urusi Kremlin kutangaza rasmi talaka ya Putin imevunja miiko ya muda mrefu kuhusu maisha ya faragha ya viongozi wa nchi hiyo. Putin kama viongozi wengine wa Urusi alikuwa amejitahidi kulinda maisha yake ya faragha kwa miaka mingi.
Kumekuwepo na uvumi kwa miaka kadhaa uliokuwa ukidai kwamba Putin alikuwa na uhusiano na bingwa wa michezo ya viungo wa Olimpiki, Alina Kabayeva, na baadhi ya repoti zimedokeza kwamba alikuwa amezaa na mwanamke huyo.    


0 comments: