Saturday 15 June 2013

USA YAPANGA KUWEKA MARUFUKU YA KUPAA NDEGE SYRIA


USA yapanga kuweka marufuku ya kupaa ndege Syria
Duru za karibu na ikulu ya White House nchini Marekani zinasema kuwa, mazungumzo ya siri yanaendelea kati ya Rais Barack Obama na makamanda wake wa jeshi ili kutafuta njia ya kuweka marufuku ya kutopaa ndege nchini Syria ili kulemaza nguvu za kijeshi za Rais Bashar Asad dhidi ya wapinzani wake. Habari zinasema kuwa Marekani huenda ikakosa kupata uungaji mkono katika Umoja wa Mataifa kuhusiana na suala hilo kwa kuzingatia kwamba Russia ina kura ya veto na inaweza kupinga jaribio lolote la kuibana serikali ya Damascus. Inasemekana kwamba Marekani huenda ikatumia kifua kuweka marufuku hiyo sambamba na kuwapa silaha nzito magaidi wanaotaka kuipindua serikali halali ya Rais Asad. Hata hivyo, Syria imesema iko tayari kukabiliana na mtu yeyote mwenye nia ya kuharibu zaidi mgogoro wa nchi hiyo. Umoja wa Mataifa na Russia pia zinapinga mpango wowote wa kutumiwa nguvu za kijeshi kutatua mgogoro wa Syria.

0 comments: