Saturday 15 June 2013

KINANA AMFUNGULIA MSIGWA KESI MAHAKAMA KUU

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amemfungulia kesi Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA) Mchungaji Peter Msigwa, kutokana na kumtuhumu kujihusisha na ujangili na biashara haramu ya pembe za ndovu.

Kinana amefungua kesi hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana na kitendo cha Mbunge huyo kutoa tuhuma hizo dhidi yake kwa nyakati tofauti nje na ndani ya Bunge, na kukataa kuzikanusha au kumuomba radhi hata alivyotakiwa kufanya hivyo (bofya hapa kurejea tamko kwa Wakili wa Kinana).

Inadaiwa kuwa Aprili 21 mwaka huu Mchungaji Msigwa ambaye ni Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii alitoa tuhuma hizo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika shule ya Msingi Mbuguni wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.

Aidha alizitoa bungeni wakati akiwasilisha hotuba ya Kambi ya Upinzani katika Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 2013/2014.
Katika hati yake ya madai aliyowasilisha mahakamani hapo kupitia kwa Wakili wake Eric Ng’mayo, amenukuu maneno aliyoyatamka Mchungaji Msigwa katika mkutano huyo.


0 comments: