Tuesday 11 June 2013

KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM KUPOKEA RASIMU YA KATIBA MPYA CHAFANYIKA JANA

 

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akiongoza kikao cha Maalum ya CCM 'Kamati Kuu' kilichokutana jana usiku mjini Dodoma kwa ajili ya kuipokea Rasimu ya Katiba mpya, iliyosomwa hivi karibuni.
 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imekutana jana tarehe 10/06/2013 chini ya Uenyekiti wa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Kikao hicho kilikuwa cha siku moja na maalum kwa ajili ya kupokea rasimu ya katiba mpya.


Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imekutana jana tarehe


10/06/2013 chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Mrisho

Kikwete. Kikao hicho kilikuwa cha siku moja na maalum kwa ajili ya kupokea
rasimu ya katiba mpya.

Kamati Kuu inaipongeza Tume ya Mabadiliko ya

Katiba nchini kwa kazi nzuri na kukamilisha kazi kwa wakati.

Kamati Kuu imepokea rasimu hiyo na kuelekeza

kuwa;

Kwa kuwa rasimu hii ni ya kwanza ambayo

inapelekwa kujadiliwa tena kwa wananchi kupitia mabaraza mbalimbali ya katiba
baada ya kuisha kwa hatua ya kutoa maoni.
 Kamati Kuu imekiagiza Chama kijipange
kuijadili rasimu hiyo ndani ya Chama kama baraza la kitaasisi la katiba na
kuwataka wanachama na wapenzi wa CCM wajitokeze kwa wingi na kushiriki kwenye
mabaraza haya.

Ushiriki huu wa CCM baada ya kupokea rasimu

umekusudia kushirikisha wanachama wetu kwenye ngazi ya tawi, wilaya, mkoa na
Taifa.

Lakini pia Jumuiya za CCM zimekusudia kushiriki

kama mabaraza ya Katiba na hivyo kuongeza ushiriki wa wanachama na wapenzi wa
CCM katika mchakato huu.

CCM kama baraza la katiba la kitaasisi

litaipitia rasimu iliyowasilishwa kifungu kwa kifungu na
kwa kuzingatia maoni ya CCM yaliyotolewa

mwanzoni kabisa mwa mchakato wa mabadiliko ya Katiba, wanachama wetu
watashiriki kutoa maoni yao.

Pamoja na kazi nzuri ya Tume ya Mabadiliko ya

katiba, Kamati Kuu inaiomba Tume hiyo kueleza vizuri mchakato mzima kutoka
rasimu ya kwanza mpaka rasimu ya mwisho ili kuondoa mkanganyiko kwa wananchi
juu ya mchakato mzima hasa baada ya rasimu ya kwanza kutoka.

Kamati Kuu inawasihi Watanzania kushiriki tena

kwenye kutoa maoni kupitia mabaraza ya katiba kwa rasimu ya kwanza, bunge
Maalum la katiba kwa rasimu ya pili na kupitia kura ya maoni kwa rasimu ya
tatu, kwa amani,utulivu na kuvumiliana ili mwisho wa siku tupate Katiba nzuri
ya nchi yetu kwa masilahi ya Watanzania walio wengi.


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Moses Nnauye, akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo mchana kuhusu kikao hicho cha Kamati Kuu ya CCM, kilichokutana jana usiku.

 Baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu, waliohudhuria kikao hicho jana usiku.

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, Mwigulu Nchemba, akiperuzi 'mambo flani' katika simu yake ya mkononi, wakati akiwa ukumbini humo kwenye Kikao cha Kamati Kuu kilichokutana jana usiku.
 Sehemu ya Wajumbe wa Kikao hicho ambao wengi wao ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

0 comments: