Friday, 7 June 2013

MWANA FA KUMFARIJI MAMA MANGWEA KWA KUFANYA SHOO


MSANII mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini, Hamisi Mwinjuma ‘MwaFA, amesema kuwa asilimia 15 ya mapato ya shoo yake ya ‘The Finest’ anatarajia kutoa pole kwa mama yake Albert Mangwea ‘Ngwair’ aliyefariki Mei 28 nchini Afrika Kusini.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgjwhzJRxl1ikOSTfFiL0IiDtmEZ8Xgznhk3SRR5T-07Z4T-3H7xH6Xsgj3BcfWhgW4r3J_TLDNEjA7n288lT376iApfDMHiyQM_m3NslFTj5nFMgr4-mVu3pUSn2SVRqaUUP0GaDWZ4YU/s640/Screen+shot+2013-05-28+at+21.13.07.png
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, MwanaFA alisema kuwa shoo hiyo ya kutimiza miaka 18 tangu aanze muziki, inatarajiwa kufanyika katikia Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam.

Alisema kuwa aliahirisha tamasha hilo ambalo lilikuwa lifanyike mwishoni mwa wiki iliyopita kutokana na kupata taarifa ya msiba huo.

Alisema kuwa anaelewa mchango wa Ngwair katika tasnia ya muziki wa Hip Hop na hivyo hana budi kutoa mchango wake wa hali na mali kwa ajili ya kumsaidia mama wa marehemu pamoja na familia nzima.

“Ninatarajia kutoa asilimia 15 ya mapato ya tamasha la The Finest kwa ajili ya kumpa mama yake Ngwair kwani alikuwa mmoja kati ya wasanii wa Hip Hip aliyekuza muziki huo nchini na hivyo lazima tutambue mchango wake,” alisema.

http://baabkubwamagazine.com/wp-content/uploads/2013/05/11.jpg
MwanaFA alisema kuwa katika tamasha hilo ambalo atalitumia kuimba nyimbo zake mpya pamoja na zile za awali, linatarajiwa kusindikizwa na wasanii mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ben Pol, Njenje, Linah, Crazy GK pamoja na AY.

0 comments: