Tuesday 18 June 2013

WABUNGE NI WABINAFSI ASEMA SPIKA ANNA MAKINDA

 



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh7z07zDFgyD_RYEoc5gjrZGyP05MrYKhJwCB9uUd_T4gVGracHaiuOCzBxMPCuTlFql1QzWBTIzb_wmmyi2DVqrpQjpNrV8aQHhjOph-jO4mFtf_vFg5bYwF_ZO2RaNU9_q-9SQyeOZGW0/s640/anne-makinda.jpgSPIKA wa Bunge, Anne Makinda amewatuhumu wabunge wenzake kwa ubinafsi unaowasababisha wasiunde mtandao wa pamoja kusimamia masuala yanayogusa maslahi ya nchi.

Makinda alitoa tuhuma hizo jana mjini hapa wakati akifunga mkutano wa siku tatu wa mwaka wa Chama cha Mabunge Afrika Wanaopambana na Rushwa (APNAC).

Alisema hivi sasa kila mbunge anaibuka na hoja yake bila kuwashirikisha wenzake ili aonekane ndiye mwanzilishi wa jambo fulani.

Kiongozi huyo alitoa tuhuma hizo alipokuwa akijibu malalamiko ya baadhi ya wadau wakiwemo wabunge, kuhusu usiri wa mikataba ambayo walitaka iwekwe wazi ili wananchi waione na kuisoma.

Alisema mikataba hiyo inapatikana kwa wabunge kupitia ofisi yake, lakini baadhi yao wamekuwa wakienda kuipitia kila mmoja kwa wakati wake badala ya kuunda mtandao wa kusaidiana na kuibana serikali pale wanapotaka kuleta hoja bungeni.

“Tatizo ninaloliona kwa Bunge langu la sasa, siku hizi ile ‘net working’ (mtandao) kati ya wabunge haipo. Maana haitoshi wewe peke yako unakwenda kusoma mkataba halafu ukaibua hoja. Utakuwa peke yako.

“Kila siku nawaambia kuwa nimekuwa mbunge tangu mwaka 1975, tulikuwa na mtandao wetu wa kuipinga serikali. Mnakaa mnajadiliana hoja kwa nguvu kabisa na ikija bungeni hakuna namna serikali inaweza kushinda,” alisema.

Aliongeza kuwa hata wakati wa kujadili miswada ya sheria, kuna baadhi ya wabunge wanakaa peke yao na kuandaa mabadiliko kisha wanayapeleka kwake ikiwa imebakia nusu saa ambapo ni kinyume na kanuni.

Alisema kuwa anapoyakataa mabadiliko hayo, wabunge husika hukimbilia kwenye vyombo vya habari kulalamika kuwa anapendelea wakati wakijua walikosea kuwasilisha mabadiliko yao.

“Mngekuwa na mtandao mngekuwa mnakuja bungeni mmekamilika. Lakini kila mtu anasimama anazungumza masuala yake ya vyama badala ya matatizo ya nchi ili aonekane kwenye TV kuwa ndiye muasisi wa hoja hiyo,” alisema.

Alisema ili wabunge waweze kupambana na rushwa, lazima wajiwekee mfumo wa maadili kwa kujitazama wao kabla ya kuwanyooshea vidole wengine.
 
Chanzo jaizmelaleo bolg

0 comments: