Friday, 7 June 2013

TANZANIA BADO INA REKODI MBAYA YA VIFO VYA WATOTO WACHANGA

IMEELEZWA kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 duniani zenye idadi kubwa ya vifo vya watoto punde baada ya kuzaliwa kati ya nchi 176 zinazokabiliwa na tatizo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mshauri wa Programu ya Afya wa Shirika la Save the Children Tanzania, Stephen Ayella, alisema vifo hivyo vinatokana na wajawazito kukosa wahudumu bora wa afya.

Alisema Tanzania inachangia asilimia mbili ya vifo vinavyotokea siku ya kwanza baada ya kuzaliwa ambavyo huchangiwa zaidi na matatizo ya uzazi kabla, wakati na baada ya mjamzito kujifungua.

Ayella alisema katika ripoti ya hali ya afya ya mama na mtoto ya mwaka 2013 Tanzania imefanya mabadiliko ya kisera katika kupanua huduma za afya kwa watoto wanaozaliwa.

Kwa mujibu wa taarifa hii, watoto 17,000 hufa muda mfupi baada ya kuzaliwa huku watoto 48,000 chini ya miaka mitano hufa kila mwaka kwa sababu mbalimbali ikiwamo utapiamlo.

Alitaja nchi zinazoongoza duniani kuwa na idadi kubwa ya vifo vya watoto punde baada ya kuzaliwa ni Somalia, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Mali na Sierra Leone.

---
 CHANZO Tanzania Daima

 

0 comments: