Saturday 15 June 2013

MJERUMANI SCHURRLE ATUA CHELSEA AKITOKEA LEVERKUSEN



Makubaliano ya kumuhamisha mchezaji wa Kijerumani, Andre Schürrle, kwenda kwenye klabu ya Chelsea ya Uingereza, yamekamilishwa.
 http://inserbia.info/news/wp-content/uploads/2013/06/Andre-Schurrle-Bayer-Leverkusen.jpg
Chelsea imetangaza kwamba hatimaye juhudi zake za kumwinda mchezaji huyo nyota huyo wa Bayer Leverkusen zimefanikiwa. Gazeti la soka la Ujerumani, Kicker, limeripoti kwamba mshambuliaji huyo ameigharimu Chelsea euro milioni 23. Makubaliano hayo yalikamilika baada ya Leverkusen kumpata mchezaji wa kuchukua nafasi ya Schürrle ambaye ni Mkorea Hueng-Min Son anayechezea Hamburg.

0 comments: