Thursday 13 June 2013

BALOZI SEIF AFUNGUA SEMINA YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI

Balozi Seif afungua semina yakuimarisha uhusiano baina ya viongozi wa kisiasa, watendaji serikalina na wajumbe wa Baraza la wawakilishi

 Mawaziri wa SMZ walioshiriki Semina ya siku mbili ya kuimarisha uhusiano baina ya Viongozi wa Kisiasa na watendaji kutoka Serikalini na Baraza la Wawakilishi  inayofanyika huko Zanzibar Beach Resort Mbweni.
Kutoka kulia kuelekea kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali  Mh Ali Juma Shamuhuna  na Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiifungua Semina ya siku mbili ya kuimarisha uhusiano baina ya Viongozi wa Kisiasa na watendaji kutoka Serikalini na Baraza la Wawakilishi  inayofanyika huko Zanzibar Beach Resort Mbweni.
 Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Mapango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa  Nchini Tanzania Bibi Andisa Mashologu akitoa salamu kwenye semina ya siku mbili ya kuimarisha uhusiano baina ya Viongozi wa Kisiasa na watendaji kutoka Serikalini na Baraza la Wawakilishi  inayofanyika huko Zanzibar Beach Resort Mbweni.
 Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu akitoa mada inayohusu  Katiba na Mgawanyo wa Madaraka katika mihimili ya Dola kwenye semina ya siku mbili ya kuimarisha uhusiano baina ya Viongozi wa Kisiasa na watendaji kutoka Serikalini na Baraza la Wawakilishi  inayofanyika huko Zanzibar Beach Resort Mbweni.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim akitoa mada  inayohusu Jukumu la Baraza la Wawakilishi katika kusimamia Serikali kwenye semina ya siku mbili ya kuimarisha uhusiano baina ya Viongozi wa Kisiasa na watendaji kutoka Serikalini na Baraza la Wawakilishi  inayofanyika huko Zanzibar Beach Resort Mbweni.
 
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ

0 comments: