Friday 7 June 2013

WAZIRI MKUU WA ZAMANI UFARANSA, MAUROY AFARIKI DUNIA




Waziri Mkuu wa zamani wa Ufaransa Pierre Mauroy amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84.
 
http://l3.yimg.com/bt/api/res/1.2/_CXMPF6NyrpZvy8PT1n0Cw--/YXBwaWQ9eW5ld3M7Y2g9Mzg5O2NyPTE7Y3c9NTEyO2R4PTA7ZHk9MDtmaT11bGNyb3A7aD0zODk7cT04NTt3PTUxMg--/http://media.zenfs.com/en_GB/News/AFP/photo_1370594395296-1-0.jpg
 
Habari za kifo chake zimetangazwa leo hii na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Laurent Fabius.Mauroy ambaye alikuwa waziri mkuu kati  ya mwaka 1981 na mwaka 1984 chini ya Rais wa kwanza Msoshalisti nchini Ufaransa Francois Mitterand alikuwa amefanyiwa upasuaji wa uvimbe wa satarani katika pafu lake hapo mwezi wa Aprili. Rais Francois Hollande ambaye yuko katika ziara rasmi nchini Japani amemuelezea Mauroy kuwa ni mtu aliyeitumikia Ufaransa wakati wa vipindi vya aina yake ambapo alichukuwa hatua za kishujaa na kuitumikia nchi yake bila kudhoofisha misingi yake muhimu. Mauroy alikuwa meya wa mji wa Lille kwa miaka 28 tokea mwaka 1973 hadi mwaka 2011.

0 comments: