Friday, 7 June 2013

CCM YA KUTANA WIKI IJAYO KUJADILI RASM YA KATIBA MPYA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa wiki ijayo kuongoza Kamati Kuu ya chama hicho kujadili Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyozinduliwa hivi karibuni.

Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana alisema msimamo wa chama juu ya rasimu hiyo utajulikana baada ya kikao hicho.
Alisema kwa sasa hawawezi kupinga wala kupongeza mpaka watakapoijadili kwa pamoja.

Alisema hayo wakati akizungumza katika mahojiano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya kufanya mazungumzo na wajumbe wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam waliowasili nchini juzi kwa malengo ya kuimarisha uhusiano na CCM.

Kwa mujibu wa Kinana, baada ya kuchambua kifungu kwa kifungu, chama hicho kitatoa msimamo wake. Alisema katika suala hilo siyo vizuri kutoa msimamo bila kushirikishana kwani bahati nzuri chama hicho kina vikao halali vya kujadili masuala mbalimbali.

Kikao hiki cha Kamati Kuu kitafanyika Jumatatu ijayo chini ya Mwenyekiti wake Rais Kikwete kisha kupata msimamo wa chama chetu, alisema Kinana.

Kinana alisema watajadili kwa kuzingatia hali halisi ya sasa kwa taifa la leo na lijalo ili kuweka kuunga mkono rasimu hiyo au kuipinga.

---

0 comments: