HATIMAYE Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, limeamua kuwafukuza
kazi askari wake 12 wanaotumiwa kujihusisha na biashara za magendo na
kuwalinda wafanyabiashara wanaokwepa kodi.
Awali kabla ya hatua hiyo kufikiwa askari 16 walikuwa wakishikiliwa katika kituo cha kati na uchunguzi uliofanyika dhidi yao wanne walibainika kutohusika na tuhuma hizo.
Tanzania Daima imedokezwa kuwa askari 12 waliofukuzwa kazi wakati wowote kuanzia sasa watafikishwa katika mahakama za kiraia kujibu mashtaka yao.
Habari za uhakika kutoka ndani ya jeshi hilo zinapasha kwamba jana askari wote 16 walikuwa wakishikiliwa katika kituo cha polisi Kati kabla ya kuhamishiwa kituo cha Kijitonyama (Mabatini) walikosomewa hukumu yao.
Askari hao walisomewa hukumu hiyo na Kamanda mpya wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, aliyeripoti kazini mwanzoni mwa wiki hii akitokea mkoani Arusha alikokuwa akishikilia wadhifa wa Mkuu wa Upelelezi Mkoa (RCO).
“Wambura kaingia kwa kishindo, kawasomea hukumu leo asubuhi wale askari waliokuwa mahabusu, wanne wameachiwa huru na wamesema wenzao wamefukuzwa kazi,” kilisema chanzo cha habari.
Tanzania Daima, iliwasiliana kwa njia ya simu na afande Wambura juu ya hukumu yake ya kuwatia kitanzini askari 12 ambapo alisema suala hilo mwenye uwezo wa kulizungumzia ni Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova.
“Hilo ni suala kubwa sana kwangu, ni la kanda, mpigie kamanda wa Kanda Maalum atakupa kila kitu unachohitaji,” alisema Wambura.
Tanzania Daima, lilipowasiliana na Kamanda Kova alihoji gazeti lilivyopata habari hizo kabla hazijafika ofisini kwake.
“Unapataje taarifa hizo kabla hazijafika kwangu wakati mimi nazisubiri? Huyo jamaa anakupaje taarifa kabla ya kufika kwangu? Mwambie aliyekupa hizo taarifa akwambie yote,” alisema.
Hata hivyo Kamanda Kova aliitaka Tanzania Daima impe muda zaidi alishughulikie jambo hilo na likiwa tayari ataliweka wazi kwa umma

0 comments:
Post a Comment