CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepanga kutoa tamko kuhusu
rasimu ya mabadiliko ya Katiba iliyotangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba.
Akizungumza
na Tanzania Daima jana Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri wa CHADEMA
John Mrema alisema kwa sasa viongozi wa juu na watalaamu wanaisoma na
kuichambua.
“Hatuwezi kutoa maoni ya juu juu
kuhusu rasimu ya katiba… ni kitu nyeti ambacho kinatakiwa kufanyiwa kazi
kwanza ili chama kitakapozungumzwa iwe kwa ajili ya manufaa ya
Watanzania wote na si ya mtu mmoja ndiyo maana kazi hii tumeikabidhi kwa
wataalam,” alisema Mrema.
Pamoja na mambo
mengi wachambuzi hao watapitia mambo yaliyokubaliwa na yaliyoachwa ili
kuionyesha tume hiyo kuwa kuna ambayo yana manufaa kwa taifa ingawa
wameyaacha.
Katika rasimu hiyo mambo
yaliyoachwa ni pamoja na serikali ya majimbo kwa sababu kuwa gharama za
kuiendeshea zitaongezeka endapo serikali tatu zitakuwapo pamoja kuweza
kufumuka mambo ya udini, malalamiko, dalili za kujitenga, ukabila na
ukanda.
Mambo mengine yaliyokataliwa katika
serikali ya muungano ni Mahakama ya Kadhi kwa maelezo kwamba nchi
washirika zinaweza kulijadili.
0 comments:
Post a Comment