Wednesday 12 June 2013

MIAKA 3 JELA KWA KUNG'ATA UUME WA MMEWE (SINGIDA)

 Mwanamke mkulima mkazi wa kijiji cha Kisana wilaya ya Iramba mkoa wa Singida Sayuni Ramadhani (42), amehukumiwa adhabu ya kutumikia jela miaka mitatu baada ya kukiri kosa la kumng’ata uume mume wake, Onesmo Nathania (42), na kubakia ngozi ndogo, nusura ukatike.

Mwendesha mashitaka mkaguzi wa polisi Vicent Ndasa, alidai mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Iramba Mrisho Mrisho, kuwa mnamo Juni 4 mwaka huu saa 12.00 jioni huko katika kijiji cha Kisana, mshitakiwa kwa makusudi aling’ata kwa nguvu uume wa mume wake na kumsababishia maumivu makali.

Ndasa amesema siku ya tukio, wanandoa hao waliporejea nyumbani kutoka kwenye klabu ya pombe za kienyeji mali ya kijiji cha Kisana, kulitokea kutokuelewana na kupelekea waanze kugombana.

Amesema wakati wanaendelea kupigana, Onesmo alizidiwa nguvu na aliangushwa chini kisha kugandamizwa
 na zipu yake ya suruali kufunguliwa na mshitakiwa ambaye baadaye alifanikiwa kuutoa uume wa mumewe kutoka ndani ya nguo ya ndani na kuutia mdomoni na ksiha kuung’ata kwa nguvu.

Mwendesha mashitaka huyo, amesema kuwa mlalamikaji, Onesmo alipiga yowe na majirani wema walifika mara moja na kisha kumkimbiza katika zahanati ya kijiji kwa ajili ya matibabu.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Ndasa aliiomba mahakama hiyo impe adhabu kali mshitakiwa ili iwe fundisho kwake na kuogofya wanawake wanaotarajia kuwafanyia unyama wa aina hii waume zao ukome.

Kwa upande wake, mshitakiwa Sayuni aliiomba mahakama hiyo imwonee huruma na kumpa adhabu nafuu kwa madai kuwa hilo ni kosa lake la kwanza toka amezaliwa na vile vile ana jukumu kubwa la kushirikiana na mume wake katika kulea idadi kubwa ya watoto walionao.

Akisoma hukumu hiyo, hakimu mfawidhi Mrisho, alisema mahATAakama yake imezingatia kwa makini maombolezo ya mshitakiwa na kufikia uamuzi wa kutoa adhabu ya kutumikia kifungo cha kwenda jela miaka mitatu.



 Na Nathaniel Limu, SINGIDA via MoBlog

0 comments: