Saturday 15 June 2013

HABARI KUTOKA MEREKANI: OBAMA AIDHINISHA SILAHA KWENDA SYRIA



Rais Barack Obama wa Marekani ameidhinisha uamuzi wa nchi yake kuwapa silaha waasi wa Syria kwa mara ya kwanza.

Uamuzi huu unakuja masaa machache, baada ya Ikulu ya Marekani kutamka kwamba ina ushahidi kamili wa utawala wa Rais Bashar al-Assad kutumia silaha za kemikali dhidi ya waasi. Ikulu hiyo imesema kuwa, sasa Marekani itatoa msaada wa moja kwa moja kwa upinzani wa Syria huku chanzo kimoja cha serikali ya Marekani kikisema kuwa msaada huo utajumuisha silaha na risasi. Uamuzi wa Marekani unafikiwa katika wakati ambapo wanajeshi wa Assad, wakisaidiwa na Hizbullah, wanasonga mbele kuelekea ngome ya wapinzani ya Aleppo.

0 comments: