Saturday 8 June 2013

POMBE YA SABABISHA MTU KUCHOMWA KISU MPAKA KIFO

— Mwendeshaji bodaboda mmoja amedungwa kisu na mkewe na kufa katika kijiji cha Kianjokoma, wilayani Embu Kaskazini kutokana na kujaribu kumnywesha pombe mwanaye wa miezi minane.

Mkuu wa polisi wa Embu Gasper Makau alisema mwanaume huyo, Kennedy Chomba, 32 inadaiwa alidungwa kisu na mkewe Lucy Wanjira 18 mwendo wa saa tano usiku,  baada ya kufika nyumbani akiwa mlevi na kutaka kumnywesha pombe mwanaye. Mwanamke huyo alijaribu kumzuia na ndipo mzozo ukazuka. Kennedy akachukua kisu na kutisha kumuua mkewe lakini mwanamke huyo alifanikiwa kukitwaa na kumdunga nacho.

Mwanamume huyo alichechemea hadi nje ya nyumba kutafuta usaidizi lakini akafa meta chache kutoka nyumbani kwake. Mkewe baada ya kuona yaliyotokea, aliwaita majirani ambao waliwaita polisi na kumkatata.
   
chanzo  SwahiliHub, Kenya 

0 comments: