Wednesday 19 June 2013

SAIDA KAROLI AKANUSHA TAARIFA YA KUZUSHIWA KUFA KWA AJALI YA BOTI

 
 Picture: Saida KaroliSaida Karoli
 
 
UPDATE: Juni 19, 2013 --- Saida Karoli amezungumza na watu kadhaa kwa njia ya simu na kueleza masikitiko yake yanayotokana na taarifa za kuzushiwa kifo.

Amewaomba watu wote wafahamu kuwa yeye ni mzima, buheri wa afya na anaendelea vyema na shughuli zake.

Ameomba taarifa ya kuwa mzima isambazwe ili kuzima uvumi na kumpunguzia kero.

-

 Jana, Juni 18, 2913 kumekuwepo na taarifa kupitia kundi pepe la majadiliano la Mabadiliko-Tanzania, zikiipoti kuwa mwanamuziki maarufu wa nyimbo za asili Tanzania na Afrika Mashariki, Saida Karoli, amefariki dunia  katika ajali ya kuzama kwa boti.Si

Kwamba, boti hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka katika kisiwa cha Goziba ilikumbwa na dhoruba ndani ya maji ya ziwa Nyanza (Victoria) na kusababisha kifo cha mwanamuziki huyo na watu wengine waliokuwa wakisafiri pamoja katika chombo hicho.

Taarifa ya Neville Meena imetoa angalizo kutafuta uhakika kwani inasemekana kuwa Saida Karoli ni mzima, yupo jijini Dar es Salaam na hajafariki dunia kama inavyoelezwa: “Nimetafuta namba yake ya simu sijaipata, ila taarifa kutoka Bukoba na ofisi ya Ofisa Utamaduni Muleba zinasema siyo kweli... kulikuwa na uvumi mwingi mjini Bukoba na Wilayani Muleba kuhusu mwanamuziki huyo kufariki lakini baadaye ikathibitika kwamba hakuwa mmoja wa abiria.” ameandika Meena.

Kuhusiana na ajali ya boti, Meena amesema, “...ni kweli kwamba kuna boti imezama katika Ziwa Victoria.”


Source: wavuti.blog

0 comments: