Sunday 16 June 2013

IRAN YAPATA RAIS MPYA HASSAN ROUANI BAADA YA UCHAGUZI MKUU KUMALZIKA

Picture
Hassan Rouhani, Rais Mpya wa Iran
Kiongozi mwenye msimamo wa kati kutoka kwenye chama cha Wahafidhina nchini Iran, Hassan Rouhani, ametangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais nchini humo.

Meya wa wa mji wa Tehran, Mohamad Baqar Qalibaf, alimeshika nafasi ya pili.

Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iran, Mostafa Mohammad-Najjar amesema katika televisheni ya Serikali ya nchi hiyo Jumamosi ya jana kuwa, Rouhani ameshinda za zaidi ya kura millioni 18, ambayo ni zaidi ya 50% ya kura zote zilizopigwa.

Najjar amesema kuwa, idadi kubwa ya raia wa nchi hiyo, zaidi ya 72% ya watu waliosajiliwa kupiga kura ambao ni milioni 50, walijitokeza kupiga kura.

Wachambuzi wa mambo wanasema ushindi huo hauna tafsiri ya moja kwa moja kuwa Serikali za nchi za nje zitabadili msimamo wao wa ujumla kuhusu dola hiyo ya Kishia ya Iran, hasa katika suala la utengenezaji wa zana za kinyuklia ambalo Rouhani alikuwa mjumbe wa kujadiliana na Jumuiya ya Kimataifa kuhusu suala hilo mwaka 2003 - 2005 ama uungaji mkono wao kwa Serikali ya Syria inayoongozwa na Rais Bashar Al-Assad.

0 comments: