Tuesday 11 June 2013

SIKU NIKIFA ASHA BARAKA NA BARAKA MSIILWA WASIFIKE KWENYE MZISHI YANGU NI" KAULI YA ALLY CHOCKY"

MKURUGENZI wa Extra Bongo Ally Choki ametoa kauli nzito kuhusu waajiri wake wa zamani, Asha Baraka na Baraka Msilwa.

Katika mahojiano yake maaalum na tovuti  ya habari za muziki na wanamuziki nchini, Saluti5, Choki alisema katika watu asiowapenda duniani ni Asha Baraka (Mkurugenzi wa ASET) na Baraka Msilwa (Mwenyekiti wa ASET). Asha Baraka na Baraka Msilwa ni mtu na kaka yake.

Kiongozi huyo wa Extra Bongo akaenda mbali zaidi kwa kusema: “Nikifa leo hii Asha Baraka na Baraka Msilwa wasije kwenye mazishi yangu, na kama watanitangulia wao na mimi sitakwenda kwenye mazishi yao.
“Nina uhakika leo hii nikipata matatizo au nikifa Asha na Msilwa watafurahi, sasa kuna haja gani ya watu kama hao kuja kwenye mazishi yangu. ASET ni kama simba wako tayari kukutafuna hadi macho, nimetafakari kwa muda mrefu sana nimevumilia mengi sana lakini nimeshindwa na sasa natamka rasmi, Nikifa wasinizike.”

Chocky ameorodhesha sababu nyingi sana za kufikia hatua hiyo lakini miongoni mwa sababu zake ni hizi tatu:
Kitendo cha Aset kumpeleka mahakamani kumdai gari; ASET kukataa kurudisha pesa za Miraji Shakashia na tatu ni ASET kutothamini michango ya wasanii walioizalishia pesa nyingi.

Chocky ansema kitendo cha Aset kumpeleka mahakamani kumdai gari ambalo walimpa mwenyewe kilimkera sana: “Mtu anapokupeleka mahakamani maana yake ni kwamba yupo tayari hata ufungwe, ukifungwa maana yake ni kila kitu kwenye maisha yako kinaharibika. Gari walinipa wenyewe na maandishi yapo kwamba nikimaliza mkataba wangu gari litakuwa la kwangu. Lakini badala yake wakanigeuzia kibao na kwenda kunidai mahakamani kwamba nimeiba gari... 

0 comments: