Tuesday 11 June 2013

MZEE MIAKA 50 AGONGWA NA BODABODA NAKUFARIKI DUNIA (KILMANJARO)

 
http://4.bp.blogspot.com/-mLylQ6em6Mk/UWKp55NJ8BI/AAAAAAAAkGk/wvEC8pNqCsk/s640/DSCF0527.JPG
Duru za habari kutoka Shimbi wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro zinasema mtu aliyefahamika kwa jina la Andrew Swai (50) amepoteza maisha yake baada ya pikipiki aliyokuwa akiendesha kugongana na lori.
 
Taarifa ya Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro, imesema kuwa tukio hilo limetokea Jumanne ya Juni 10 majira ya 10 jioni maeneo ya Shimbi-Kati barabara ya Mwika-Tarakea.

Ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Mitsubishi Fuso lenye namba za usajili T 530 AEK lililokuwa likiendeshwa na Deodath Tesha (30) mkazi wa Shimbi ambalo liligongana na pikipiki yenye namba T 927 BRF aina ya Skygo.

Katika ajali hiyo marehemu alipata majeraha kichwani na kupelekwa katika hospitali ya Huruma ambapo alikufa muda mchache wakati akipatiwa matibabu.

Chanzo cha ajali hiyo ni kuwa marehemu alikuwa akitokea barabara moja ya mtaa na kuingia barabara kuu bila kuchukua tahadhari ya kuangalia kushoto na kulia na kuingia moja kwa moja  hali iliyosababisha  ajali hiyo.
Mwandishi: YOHANA GERVAS, Moshi-Kilimanjaro
Mhariri: ABDUL MARWA

0 comments: