Tuesday 11 June 2013

LWAKATARE WA CHADEMA APATA MDHAMAN LEO

Mkurugenzi wa Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare amepata ruhusa ya kuachiwa kwa dhamana ya Shilingi milioni kumi, kuwa na wadhamini wawili wanaotambulika, kuikabidhi mahakama hiyo pasi yake ya kusafiria na kutokusafiri nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila taarifa.

Masharti hayo ni kwa mujibu wa amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaa
Kwa sasa kesi imesimama mpaka saa nane mchana baada ya waliofika kumtolea dhamana kukosa baadhi ya vielelezo hivyo kwenda kuvifuatilia. Baadhi ya wanachama wa CHADEMA wapo nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakisubiri muda utimie ili wajue hatima ya kiongozi wao. Mwandishi wa GPL aliyepo mahakamani hapo alipoongea na wanachama hao wanadai kuwa leo lazima kieleweke na watahakikisha wanaondoka na kiongozi wao maana amesota sana rumande.

chanzo gazeti la MWANANCHI:

0 comments: