Saturday 1 June 2013

: MWALIMU KORTINI KWA KUMWEKA UNYUMBA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI




http://1.bp.blogspot.com/-nknbe6JQTyk/T2-ihTNOqEI/AAAAAAAAAj0/RZFkC-HsqAE/s400/Police1.jpgJESHI la Polisi mkoani Rukwa linamshikilia Mwalimu  Ased Job (31) kwa  kumtorosha  mwanafunzi  wa  kike mwenye umri wa miaka 17  kisha kuishi naye kinyumba kwa zaidi ya miezi  miwili sasa.

Mwalimu  huyo  ambaye  anafanya  kazi  katika Idara  ya Elimu  katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga  anatuhumiwa kuishi  na  mwanafunzi  huyo  anayesoma  kidato  cha pili  kama  mkewe  kwa kipindi  hicho  chote.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Peter Ngusa,  akithibitisha kutokea kwa tukio hilo alisema lilitokea  Februari  mwaka  huu  baada ya mtuhumiwa kumtorosha  mwanafunzi  huyo na kumpeleka  mkoani Mbeya kisha kufanya taratibu za uhamisho kwa lengo la kumhamishia mkoani Mbeya ili akaishi naye huko.

“Baada ya kukamilisha uhamisho  huo mwanafunzi huyo alihamia mkoani Mbeya kisha akaanza kuishi  na mwalimu  huyo  kinyumba  hadi  mwisho  mwa  Mei  mwaka huu  alipomrejesha  mjini  Sumbawanga  na kuendelea  kuishi  naye kinyumba kisha baadaye kukamatwa,” alisema.

Kwa  mujibu  wa  Ngusa kukamatwa  kwa  mtuhumiwa huyo  kunatokana na taarifa za siri  za  wasamaria  wema  na kwamba anatarajiwa kufikishwa  mahakamani  muda  wowote  mara baada ya  ya upelelezi  wa  awali  dhidi  ya shauri  lake kukamilika.
CHANZO: TANZNAIA DAIMA

0 comments: