Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi Bw.
Morice Oyuke kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (katikati) akizungumza na
Waandishi wa habari kuhusu ukuaji wa Pato la Taifa kwa robo mwaka ya
tatu ya mwaka 2013 ambapo katika kipindi cha Julai – Septemba, 2013 Pato
la Taifa kwa bei za soko liliongezeka kwa kasi ya asilimia 6.5
ikilinganishwa na asilimia 7.2 kwa kipindi kama hicho mwaka 2012. Kulia
kwake ni Bw. Juma Omary, Mchumi Mkuu kutoka Ofisi ya Rais Tume ya
Mipango na kushoto ni Bw. Daniel Masolwa Meneja Takwimu za Pato la Taifa
kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
Baadhi ya Waandishi wa Habari
wakimsikiliza Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi Bw. Morice Oyuke kutoka
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (katikati) akizungumza kuhusu ukuaji wa Pato
la Taifa kwa robo mwaka ya tatu ya mwaka 2013 katika ukumbi uliopo Ofisi
ya Rais Tume ya Mipango, Dar es Salaam.
(Picha na Veronica Kazimoto)
0 comments:
Post a Comment