Serikali ya Uingereza kwa mara ya kwanza
imetambua mateso na ukandamizaji vilivyofanywa na maafisa wake wa kikoloni
katika operesheni za kuzima uasi wa Mau Mau nchini Kenya mnamo miaka ya 1950.
Hata
hivyo nchi hiyo imesema haiwajibiki kutokana na vitendo hivyo vilivyofanywa na
watawala wa kikoloni, na badala yake imekubali kulipa fidia ya kiasi cha euro
milioni 23 kwa wazee takribani 5000 nchini Kenya ambao waliathiriwa na vitendo
hivyo. Kila mmoja wa wazee hao atapata kiasi cha Euro 4,700.
Waziri
wa mambo ya nchi za nje wa Uingereza William Hague aliomba radhi kwa niaba ya
serikali yake, kwa kile alichokiita uvunjaji wa haki za binadamu uliovuruga
mchakato wa kupigania uhuru wa Kenya. Alisema Uingereza inavilaani vitendo
hivyo kwa nguvu zote.
0 comments:
Post a Comment