Sunday 2 June 2013

MWILI WA NGWAIR KUTOWASILI TENA LEO HII




Kamati ya msiba ya mwanamuziki Albert Mangwea, imeleta taarifa kwamba mwili wa Ndugu  yetu Albert Mangwea hautoweza kufika siku ya jumapili ya tarehe 2/ 06/2013 kama ilivyo taarifa hapo awali, hii ni kutokana na sababu  zilizokuwa nje ya uwezo wetu.
Kwa sasa tunasubiri taarifa kamili kutoka kwa wenzetu/wawakilishi  wetu waliopo nchini Afrika Kusini, mara tutakapopata taarifa hizo  tutawafahamisha zaidi.
Tunaomba radhi watanzania wote kwa usumbufu wote  uliojitokeza  tushirikiane na uvumilivu kwa hili.

0 comments: