Tuesday, 5 August 2014

BILIONEA WA ARSENAL AITABIRIA KLABU KUINGIA ‘ZAMA ZA MATAJI!’

  TUESDAY, 05 AUGUST 2014 21:35

PrintPDF
WENGER-FA_CUPMMILIKI wa Pili kwa Hisa nyingi Klabuni Arsenal, ALISHER USMANOV, ametabiri kuwa Klabu yao sasa inaingia zama za kutwaa Mataji.
Msimu uliopita Arsenal ilimaliza ukame wake wa kutotwaa Kombe lolote kwa kunyakua FA CUP Uwanjani Wembley baada ya kuichapa HULL CITY Bao 3-2.
Alisher Usmanov, Bilionea kutoka huko UZBEKISTAN, amesema mafanikio mengine makubwa yapo njiani.
Usmanov ametamka: “Nadhani tunaingia zama mpya za Arsenal kushinda Vikombe. Hilo ni muhimu sana kwa Soka. Klabu iko kwenye nafasi nzuri kufanya hivyo!”

ALISHER USMANOV
-Ni Tajiri mwenye thamani ya Pauni Bilioni 16 inayotokana na uvunaji Migodi ya Chuma.
-Alinunua Hisa za Arsenal Mwaka 2007 kutoka kwa aliekuwa Makamu Mwenyekiti David Dien za thamani ya Asilimi 14.65
-Februari 2012 aliongeza Hisa zake Arsenal kufikia Asilimia 30
-Julai 2012, aliiponda Arsenal kwenye Barua ya wazi kwa kukosa dira.

Usmanov, ambae kwa mujibu wa Jarida la Forbes ni Mtu wa 42 kwa Utajiri Duniani, amefafanua kuwa ukame wao wa kukosa Vikombe kwa Miaka 9 ungeepukika endapo Arsenal ingekwepa kujiingiza kwenye Deni la kujenga Uwanja wa EMIRATES.
Amefafanua: “Bodi na Wamiliki Hisa wakubwa wa Arsenal waliamua kujiingiza kwenye Deni wakati ule na Arsenal ikajikuta ikipitisha karibu Miaka 10 bila kutwaa Ubingwa na UEFA CHAMPIONZ LIGI. Uwanja ule umepatika kwa Madeni ambayo yanalipwa kwa Mapato ya Mechi pamoja na njia nyingine.”

0 comments: