WACHEZAJI 16
kati ya 34 wa kikosi cha Maboresho ya Timu ya Taifa (Taifa stars)
wamechaguliwa kutoka kwenye kambi iliyokuwa ikifanyika katika Uwanja wa
Chuo cha Ualimu Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya .
Kikosi
hicho kimetangazwa leo jijini Mbeya na Kocha Msaidizi, Salum Mayanga,
aliyekuwa na timu hiyo katika Mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika
katika ukumbi wa Hoteli ya Hill View iliyopo mjini humo.
Mayanga aliwataja wachezaji hao kuwa ni Mlinda mlango Benedict Tinoko Mlekwa kutoka Mara.
Walinzi wa kati: Emma Namwondo Simwanda kutoka Temeke na Joram Nason Mgeveja kutoka Iringa.
Walinzi pembeni
: Omari Ally Kindamba kutoka Temeke, Edward Peter Mayunga kutoka
Kaskazini Pemba na Shirazy Abdallah Sozigwa kutoka Ilala,viongo wa
Ulinzi ni Yusufu Suleiman Mlipili na Said Juma Ally kutoka Mjini
Magharibi.
Viungo
Washambuliaji: Abubakar Ally Mohamed kutoka Kusini Unguja na Hashimu
Ramadhani Magona kutoka Shinyanga, na Viungo wa pembeni ni Omari
Athumani Nyenje kutoka Mtwara na Chunga Said Zito kutoka Manyara.
Washambuliaji:
Mohammed Seif Said kutoka Kusini Pemba, Ayubu Kassim Lipati kutoka
Ilala, Abdurahman Othman Ally kutoka Mjini Magharibi na Paul Michael
Bundara kutoka Ilala.
Madadi
aliongeza kuwa katika kikosi hicho pia wamechaguliwa wachezaji wawili
waliojiunga na Timu ya Taifa ya wenye umri chini ya Miaka 20 ambao ni
Mbwana Mshindo Musa kutoka Tanga na Bayaga Atanas Fabian kutoka Mbeya.
Aidha
Kocha huyo alisema wachezaji wengine walioachwa wataendelea kuwa kwenye
uangalizi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF) kwa sababu mpango wa
maboresho ya timu ya Taifa ni endelevu.
Alisema
Kambi ya timu hiyo ilianza Machi 22, Mwaka huu na kuhitimishwa Aprili
17, mwaka huu kwa awamu ya kwanza ambapo wachezaji hao watajiunga na
kikosi cha Timu ya Taifa cha Awali kwa ajili ya maezo ya mechi ya
Kirafiki kisha watarudi tena wilayani Rungwe kwa ajili ya Kambi ya awamu
ya Pili.
chanzo: shaffih dauda.com
0 comments:
Post a Comment