Katika taarifa yake kwa umma jana jioni, TMA imesema maeneo ambayo yataathiriwa na mvua hizo za kuanzia leo ni Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na mikoa ya Tanga, Pwani na Dar es Salaam.
Mbali ya vifo hivyo, mvua hizo zilisababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara hasa madaraja.
Mawasiliano ya barabara kati ya Mkoa wa Dar es Salaam na mingine nchini yalikatika kwa siku mbili baada ya barabara zake zote zinazouunganisha na maeneo hayo ama kuharibiwa vibaya na mafuriko au kujaa maji na kushindwa kupitika.
Taarifa hiyo ya TMA imesema mvua hizo zinatarajiwa kuwa kubwa kwani zitazidi milimita 50 katika saa 24.
"Wakazi wa maeneo hatari, watumiaji wa bahari pamoja na mamlaka zinazohusika na maafa, wanashauriwa kuchukua tahadhari stahiki," ilisema taarifa hiyo
0 comments:
Post a Comment