Mwemyekiti wa Taasisi ya Catherine
Foundation ya mjini Arusha ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum,
Catherine Magige (kushoto) akikabidhi masaada wa unga wa sembe kwaajili
ya uji wa wanafunzi shule ya msingi Levolosi. Wanao pokea ni Mwenyekiti
Kamati ya Shule, Edward Ngomuo (kulia) Mwalimu Mkuu Shule ya Luvolosi,
Elisante Kaaya na Mwalimu wa Chakula shuleni hapo, Frida Mallya.
JAMII imetakiwa kuwa na moyo wa
kujitolea na kusaidia makundi mbalimbali yenye uhitaji katika jamii hasa
wanawake na watoto ili kujenga taifda lenye matumaini na amani.
Hayo yamesemwa jana na Mwenyekiti wa
Taasisi ya Catherine Foundation, ya jijini Arusha, Catherine Magige
wakati akikabidhi msaada wa unga wa sembe na sukari kwaajili ya
kuwapikia uji wanafunzi zaidi ya elfu moja katika shule ya Msingi
Levolosi ya mjini hapa kwa muda wa mwezi mmoja.
Magige ambaye pia ni Mbunge wa Viti
Maalum (UVCCM) mkoa wa Arusha, amesema kila mtu anapswa kujipima kwenye
mizani ya ubinadamu, kujitafakari na pia kujiuliza maswali magumu kwenye
nafsi yake, kwamba, katika kipindi kifupi cha uhai wake, ameacha nyuma
matunda ya aina gani.
“Tunapaswa tusambaze mbegu za
matunda ya amani na upendo na si mbegu za machafuko…kwani ndio mbegu
ambazo sote tunapaswa kuzisambaza na kuzipanda ili kujenga taifa lenye
matumaini na amani,”alisema Magige.
Ni ukweli usio pingika kuwa watoto
wetu hawa tusipo wawezesha kupata elimu sasa basi tutakuwa
tumejingeneneazea wenyewe taifa la watu mbumbumbu na wasio na ujuzi wa
kufanya jambo lolote jema na matokeo yake wataishia katika magenge ya
uhalifu na watumiaji wa madawa ya kulevya.
Magige amesema ili watoto wafanye
vizuri darasani wanahitaji kushiba na si familia zote zinamudu kuwapa
chakula watoto wao kabla ya kwenda shule hivyo taasisi yake ya Catherine
Foundation imeona ichangie kulisha watoto hao kwa mwezi mmoja.
“Sisi kama wazazi hatuna budi
kusaidia wazazi wengine ambao wanania njema na watoto walio wazaa
isipokuwa uwezo ndio unawakwamisha katika kutimiza malengo yao ya
kuwasaidia watoto wao katika elimu,” alisema Magige.
Aidha amesema utaratibu wa kuwapa
watoto chakula shule utaongeza kiwango cha usikivu wa wanafunzi darasani
na kuongeza ufaulu huku ukupunguza tatizo la utoro mashuleni ambalo
limekithiri katika shule nyingi nchini.
“Kufanya hivi situ watoto watakuwa
wasikivu darasani bali hata kuchangia kwa kiwango cha ufaulu darasani na
ni wazi kuwa hata mahudhurio yataongezeka shuleni hapa,” alisema
Magige.
Pia amewataka wanafunzi wanafunzi
kukazania masomo yao darasani, kudumisha nidhami mingoni mwao huku
akiwataka walimu kutimiza wajibu wao ipasavyo kwa kuwapa elimu bora na
malezi stahiki watoto hao na maadili mema.
Mapema katika hotuma yake Mwalimu
Mkuu wa shule ya Msingi Levolosi, Elisante Kaaya alisema shule hiyo ina
wanafunzi 1,029 na gharama za kuwalisha kwa mwaka zinakadiriwa kuwa
zaidi ya Sh Milioni 10.
Aidha Mwalimu Kaaya alisema kuwa ili
kufanya zoezi hilo la kuwapa uji au chakula wanafunzu linaendelea
wameazimia kuwashirikisha wazazi na wadau wengine wa elimu ili uwe
endelevu na wenye kuleta tija.
Ofisa wa Catherine Foundation Lucy Bongole akizungumza jambo kabla ya makabidhiano kuanza.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi
Levolosi, Elisante Kaaya akitoa maelezo ya shule hiyo na mpango wa
kuwapa uju wanafunzi wanafunzi 1,029 na gharama za kuwalisha kwa mwaka
zinakadiriwa kuwa zaidi ya Sh Milioni 10.
Juice zikigawiwa kwa wanafunzi.
Mwenyekiti wa Shule ya Msdingi Levolosi ya jijini Arusha, Edward Ngomuo akisema neno.
Mwenyekiti wa Catherine Foundation na Mbunge wa viti Maalum Arusha, Catherine Magige akigawa juice kwa wanafunzi.
Mwenyekiti wa Catherine Foundation na Mbunge wa viti Maalum Arusha, Catherine Magige akizungumza.
Mwemyekiti wa Taasisi ya Catherine
Foundation ya mjini Arusha ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum,
Catherine Magige (wapili kushoto) akimuweka katika kiti maalum cha
magurudumu, motto mlemavu Hassan Ramadhani (10) mkazi wa Luvolosi mjini
Arusha jana. Wanaoshuhudia ni mama mzazi wa motto huyo, Hadija Hassan na
Mwalimu Mkuu Elisante Kaaya wa Shule ya Msingi Luvolosi.
Mwemyekiti wa Taasisi ya Catherine
Foundation ya mjini Arusha ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum,
Catherine Magige (kushoto) akikabidhi masaada wa unga wa sembe kwaajili
ya uji wa wanafunzi shule ya msingi Luvolosi ya mjini Arusha jana.
Anaeshuhudia ni Mwalimu Mkuu Elisante Kaaya.
Wazazi na walimu wakipokea unga na sukari
wanafunzi nao wakipokea
Wawakilishi wa wazazi wakipokea msaada huo.
Mwalimu wa Chakula shuleni hapo, Frida Mallya akitoa neno la shukrani kwa taasisi ya Catherine Foundation.
Mwenyekiti wa Catherine Foundation, Catherine Magige akiagana na wanafunzi.
0 comments:
Post a Comment