Na Samwel Ndoni Mbeya,
WAKATI takwimu za jeshi la
polisi mkoani Mbeya zikionesha matukio ya mauaji katika kipindi cha mwezi
January mpaka juni mwaka huu, yalikuwa ni 135, huenda idadi hiyo ikaongezeka
katika kipindi kijacho kama hiki kutokana na kuongezeka kwa visa hivyo mkoani
hapa.
Hali hiyo inatokana na
vitendo vya wananchi kujichukulia sheria mkononi kuzidi kushika kasi licha ya
serikali na mashirika mbalimbali kukemea vitendo hivyo, kufuatia watu wawili kuuawa kutokana na wivu wa kimapenzi wilayani
Chunya.
Tukio hilo limetokea katika
kitongoji na kijiji cha Magamba wilayani humo ambapo mwanamke mmoja
aliyefahamika kwa jina la Neema Mbuzi mkazi wa kitongoji hicho aliuawa na mume
wake kwa kukatwa mapanga baada ya kumkuta
akiwa na mwanaume mwingine asiyefahamika wakiwa nyumbani kwake wakivunja
amri ya sita.
Imeelezwa kijijini hapo kuwa
mume wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Msafiri Shitindi alimfumania mkewe
majira ya saa sita usiku ambapo hata hivyo mwanaume aliyeshikwa ugoni
alikimbia.
Aidha baada ya Mgoni huyo
kukimbia mtuhumiwa alimkamata mkewe na kuanza kumshambulia kwa kumtata mapanga
sehemu mbalimbali za mwili wake na kusababishia kifo chake.
Hata hivyo siku mbili baadae
ndugu wa marehemu Neema aliyefahamika kwa jina la Mlawa alimuua mtuhumiwa kwa
kosa la kumuua ndugu yake.
Akithibitisha kutokea kwa
tukio hilo kwa niaba ya mwenyekiti wa kitongoji hicho mjumbe wa serikali ya
Kitongoji cha Magamba Fikiri John
amesema kuwa mtuhumiwa Mlawa anashikiliwa na polisi kituo cha Mkwajuni
kwa mahojiano zaidi.
0 comments:
Post a Comment