Msemaji wa Hazina Capital, Rachel Ndauka (kulia) na William Joseph (kushoto) wakiongea na wanahabari (hawapo pichani).
Hazina
Capital tunapenda kujitambulisha/kuwatangazia Watanzania juu ya soko
jipya la biashara litakalojumuisha wafanyabiashara wa bidhaa za aina
mbalimbali kutoka Kariakoo na kuwapa nafasi ya kuonyesha pamoja na kuuza
bidhaa zao Coco Beach ambalo tumeliita ‘Kariakoo at Coco Beach’ linalotarajiwa kuanza kuanza Machi 29 na 30 mwaka huu na kila mwisho wa wiki ya mwisho wa mwezi.
Soko hili
litatatoa nafasi pia kwa wananchi ambao huwa hawaendi Kariakoo au hata
wanaoenda, kununua bidhaa zinazopatikana Kariakoo katika ufukwe huo wa
bahari na kwa bei ileile na hata ya chini zaidi.
Pia watu wanaweza kuja na familia zao kwa sababu kutakuwa na vitu vingi kama michezo ya watoto na n.k.
Lengo la
soko hili siyo kuwafanya watu wanunue tu, bali pia kuwasogezea karibu
zaidi wananchi huduma ili waweze kupata mahitaji yao katika mazingira
mazuri ya utulivu, ya furaha na usalama.
Pia lengo
letu ni kuendeleza na kukuza wafanyabiashara pamoja na kupanua zaidi
masoko yao lakini pia kuwawezesha kufikia malengo na mafanikio na
kulitangaza soko letu maarufu la Kariakoo, Tanzania.
Hazina
Capital inapenda kuwashukuru waandaaji wenza ambao ni Ndauka Promotion
na Real Stars pamoja na Hazina Lounge kuturuhusu kutumia mahali hapa.
Tunapenda kuvishukuru vyombo vya habari kwa ushirikiano.
0 comments:
Post a Comment