Na Riziki Mashaka.
Kocha wa Machester City, Manuel
Pellegrini amesema anapata kazi kubwa kupanga kikosi cha kwanza
kitachokumbana na timu ya Sunderland katika mchezo wa fainali za kombe
la Capital One utakaochezwa siku ya jumaapili, 2/3/2014.
Kocha huyo raia wa chile amesema timu
yake ilikumbwa na idadi kubwa ya majeruhi ambao mpaka sasa wamepona na
wapo tayari kuingia dimbani, baadhi ya wachezaji waliokuwa majeruhi ni
kama Sergio Aguero, Micah Richards, Fernadnho na Samir Nasri, ambaye
amepata kucheza baadhi ya mechi katika kipindi kifupi cha siku chache za
mechi zilizopita.
Kauli ya kocha huyo imetokana na
sasabu kuwa timu yake ina wachezaji wengi mahiri katika baadhi ya safu,
hali ambayo imepelekea uwepo wa vikosi viwili na kumpa tabu raia huyo wa
chile kupanga kikosi cha kwanza, mpaka sasa timu hiyo ina jumla ya
washambualiaji wanne kama Edin Dzeko, Alvaro Negredo, Sergio Aguero na
Jovetic, hali hiyo inampa tabu kocha huyo kupanga timu ya kwanza hasa
katika mchezo wa fainali ya kombe la Capital One Cup utakaochezwa
jumaapili ya wiki hili.
Siku ya Ijumaa, UEFA ilimpa adhabu
kocha huyo kwa kuonesha utovu wa nidhamu baada ya kupinga maamuzi ya
refa na kudai kuwa refa huyo akufata maadili na kanuni za usawa katika
mchezo huo ulioshuhudia Barcelona ikiitandika Man City katika uwanja
wake wa nyumbani (Etihad) kwa jumla ya magoli 2-0 katika mtanange wa
hatua ya kwanza ya klabu bingwa ya ulaya.
0 comments:
Post a Comment