Sunday, 2 March 2014

KAWAMBWA AKERWA DARAJA LA TANO KUITWA SIFURI

 
kawambwapx_3ff8e.jpg
Dk. Shukuru Kawambwa, aliyasema hayo jana mjini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Dodoma. Waziri wa Elimu na Mafunzo yaUfundi, Dk Shukuru Kawambwa ameelezea kukerwa na daraja la tano katika muundo mpya wa kupanga matokeo, kuitwa sifuri.
Dk. Shukuru Kawambwa, aliyasema hayo jana mjini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Alivishutumu vyombo vya habari kwa kuchanganya alama na madaraja yaliyopo katika muundo mpya wa kupanga matokeo ya mitihani nchini.
Alisema kwa muundo mpya, daraja sifuri ni kati ya pointi 48 na 49 ambayo inapatikana baada ya mtahiniwa kupata alama F kwa masomo yote saba.
"Ndugu zangu waandishi wa habari, kitu ambacho hamkufanya haki kwa Watanzaniasafari hii, ni ile kuliita daraja la tano kuwa ni sifuri mkalazimisha na mimi kumwagiza Katibu Mkuu abadilishe na kuita daraja sifuri," alisema na kuongeza:
"Unakuaje na daraja la kwanza, la pili, la tatu, la nne lakini unapofika la tano unaita sifuri katika namna ambavyo waandishi wa habari walipenda."
Dk Kawambwa alisema vyombo vya habari vimekuwa vikipenda taswira ya nchi ionekane kuwa ni kufeli. "Lakini ninachosema ni kwamba, pointi ni zile zile tulichoondoa ni daraja la tano."
Chanzo, mwananchi

0 comments: