Golikipa wa zamani wa Manchester United Peter Schmeichel anaamini David Moyes ni mtu sahihi kabisa kuiongoza klabu hiyo ya Old Trafford.
Mabingwa watetezi wa EPL wamekuwa na msimu mbaya zaidi katika kipindi
cha miaka 20 lakini Schmeichel anaamini kocha wa zamani wa Everton sio
tatizo linalopelekea timu kufanya vibaya.
Golikipa huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Denmark kaiambia Sky Sports News kwamba Moyes ndio kocha sahihi, lakini akamwambia kocha huyo afanye mabadiliko makubwa katika kikosi.
“Nadhani David ni chaguo sahihi kabisa, ameonyesha uwezo wake, ana
nia ya dhati na hali ya kupambana, anaweza kukaa sehemu kwa muda mrefu –
alionyesha hizi sifa alipokuwa Everton, United inahitaji kocha ambae
atakaa na timu kwa muda mrefu lakini msimu huu umekuwa mgumu kwake’
“Atajifunza mwenyewe vitu vingi ndani ya muda, kila mtu atajifunza
namna ya kuwa bora na timu itakuwa imara zaidi, nafikiri anahitaji
kusajili wachezaji kadhaa wengine – sijui wangapi ila anahitaji
wachezaji lakini vilevile naamini anahitaji kuwaondoa wachezaji wengine
kwenye timu kwa sababu kuna wachezaji wengi ambao kiukweli
wanamuangusha’
“Kuwa mchezaji wa Manchester United ,
inaamanisha kubeba majukumu, inabidi ujitoe na kuipigania timu, siku
zote hata kama mambo yanaenda visivyo, inabidi uendelee kujaribu,
nadhani mwishoni mwa msimu ujao wapo wachezaji watakaondoka”
0 comments:
Post a Comment