Wednesday, 5 March 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI NG’OMBE 30 WAIBWA KATIKA KIJIJI CHA STAMICO


DSC00207 
“PRESS RELEASE” TAREHE 05.03.2014. 
·         NG’OMBE 30 WAIBWA KATIKA KIJIJI CHA STAMICO WILAYANI CHUNYA.
·         MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI WILAYANI CHUNYA.
·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU WAKIWA NA NOTI BANDIA.
·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA MAFUTA – DIESEL MALI INAYODHANIWA KUWA YA WIZI.
·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA MAFUTA – DIESEL YANAYODHANIWA KUWA YA WIZI.
·         WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU.
·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LATEKETEZA SHAMBA LA BHANGI LENYE UKUBWA WA HEKARI MOJA WILAYANI CHUNYA.
·         WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA BHANGI.
NG’OMBE 30 WAIBWA KATIKA KIJIJI CHA STAMICO WILAYANI CHUNYA.
NG’OMBE 30 MALI YA MIHAMBO PAUL (34) MFUGAJI, MKAZI WA KIJIJI CHA STAMICO WALIIBWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 01.03.2014 MAJIRA YA SAA 17:00HRS JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA STAMICO, KATA YA MKOALA, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA  CHUNYA WAKATI MIFUGO HIYO IKIWA MALISHONI BILA MSIMAMIZI. THAMANI HALISI YA NG’OMBE HAO NI TSHS.15, 000,000/=. MSAKO MKALI UNAFANYWA ILI KUWABAINI WALE WOTE WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIOPO WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AU MIFUGO HIYO AZITOE KWA JESHI LA POLISI/MAMLKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO. 
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI WILAYANI CHUNYA. 
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA VENANCE SERA (70), MKAZI WA KIJIJI CHA UPENDO ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA PIKIPIKI ISIYOFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA CHALYA KASEMA. AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 04.03.2014 MAJIRA YA SAA 18:00HRS JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA UPENDO, KATA YA MAMBA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA.  MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA PIKIPIKI MARA BAADA YA TUKIO. JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA/KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU KUWA MAKINI WANAPOTUMIA BARABARA HASA KWA KUTEMBEA PEMBEZONI MWA BARABARA NA KUVUKA KATIKA SEHEMU ZENYE VIVUKO [ZEBRA CROSSING] ILI KUEPUKA AJALI. 
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU WAKIWA NA NOTI BANDIA. 

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU 1. TIMOTH MGINA (27) MKAZI WA SIMIKE – MBEYA 2. ALEX FUGAL (25) MKAZI WA MLOWO – MBOZI NA 3. LUSEKELO STEVEN (20) MKAZI WA IWAMBI – MBEYA WAKIWA NA NOTI BANDIA 13 KILA MOJA IKIWA NA THAMANI YA SHILINGI 10,000/= SAWA NA SHILINGI 130,000/= ZENYE NAMBA BL-6882315 NOTI 3, BX 83652992 NOTI 7 NA BX 576441 NOTI 3. WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 04.03.2014 MAJIRA YA SAA 18:13HRS JIONI HUKO KATIKA ENEO LA RUJEWA, KATA NA TARAFA YA RUJEWA WILAYA YA MBARALI. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAENDELEA DHIDI YAO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA MAKINI NA MATUMIZI YA  PESA HASA NOTI ILI KUEPUKA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MTU/MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA YA NOTI BANDIA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE. 
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA MAFUTA – DIESEL MALI INAYODHANIWA KUWA YA WIZI. 
 

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SOLOMON STEVEN (36) MFANYABIASHARA, MKAZI WA MAKONDEKO AKIWA NA MAFUTA AINA YA DIESEL UJAZO WA LITA 15 MALI IDHANIWAYO KUWA YA WIZI.MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO MAALUM ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 03.03.2014 MAJIRA YA SAA 17:00HRS JIONI HUKO KATIKA ENEO LA MAMA JOHN, KATA YA ILOMBA, TARAFA YA IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA SHUGHULI HIZI KWANI NI VITUO VYA MAFUTA NDIVYO VYENYE LESENI YA KUFANYA SHUGHULI HIZI. PIA NI HATARI KWA MAISHA YA WATU WANAOISHI MAENEO YA KARIBU PA.LE ITOKEAPO AJALI YA KULIPUKA. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO YAO KWA JESHI LA POLISI JUU YA SHUGHULI WANAZOFANYA ILI WAWEZE KUFUATILIWA KWA KARIBU ZAIDI. 
WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU.

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI 1. WILLIAM FROLIAN (25), MFANYABIASHARA NA 2. LEA MATHIAS (35) MFANYABIASHARA WOTE WAKAZI WA MKWAJUNI WAKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI VIROBA AINA YA  BOSS PAKETI 25. KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 04.03.2014 MAJIRA YA SAA 16:30HRS JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAWENI, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA WAKIWA WANAUZA POMBE HIZO KATIKA KIBANDA CHAO. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA KUACHA KUUZA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI/USAMBAZAJI WA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO. 

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LATEKETEZA SHAMBA LA BHANGI LENYE UKUBWA WA HEKARI MOJA WILAYANI CHUNYA. 
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LIMETEKETEZA SHAMBA LA BHANGI LENYE UKUBWA WA HEKARI MOJA PAMOJA NA BHANGI. KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 04.02.2014 MAJIRA YA SAA 15:20HRS ALASIRI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA ILINDI, KIJIJI CHA MAZIMBO, KATA YA  MATWIGA, TARAFA YA  KIPEMBAWE WILAYA YA  CHUNYA ASKARI  POLISI  WALIKUTA SHAMBA HILO LA BHANGI LINALOMILIKIWA NA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA MASASILA AMBAYE ALIKIMBIA MARA BAADA YA  KUWAONA ASKARI. BHANGI HIYO ILIVUNWA NA KUTEKETEZWA. JUHUDI ZA KUMSAKA MTUHUMIWA ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA ULIMAJI/USAMBAZAJI/UUZAJI WA DAWA ZA KULEVYA ILI WAKAMATWE NA SHERIA KALI ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO. 

WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA BHANGI. 
WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. NORBERT WILLIAMSON (23) FUNDI SEREMALA, MKAZI WA MBUNGANI NA 2. SHAIBU HASSAN (22) MWANAFUNZI  NA MKAZI WA MAMA JOHN  – MBEYA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA BHANGI UZITO WA GRAM 3.5. WATUHUMIWA KWA PAMOJA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 04.03.2014 MAJIRA YA SAA 12:30HRS MCHANA HUKO KATIKA ENEO LA MIKOROSHINI, KATA YA KYELA KATI, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.  
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Related Posts:

0 comments: